Unknown Unknown Author
Title: KATIBU WA CUF WILAYA YA LINDI AJIUZURU UONGOZI WAKE WA CHAMA HICHO, ATAJA SABABU HIZI HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Abdulaziz Video,Lindi Katibu wa Chama cha wananchi (CUF) wilaya ya Lindi mjini, Abubakar Taher ametangaza kujivua nyadhifa alizonazo...
 Abubakar Taher
Na Abdulaziz Video,Lindi
Katibu wa Chama cha wananchi (CUF) wilaya ya Lindi mjini, Abubakar Taher ametangaza kujivua nyadhifa alizonazo, ikiwemo uenyekiti wa tawi la Gulf manispaa ya Lindi kwa madai mbalimbali, yakiwemo Uvunjwaji wa katiba ya Chama hicho unaofanywa na Mwenyekiti wake ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini Salum Barwany

Akizungumza katika Ofisi za Klabu ya waandishi wa Habari Lindi liyopo mitaa ya Karume na Eliet, Abubakar Taher amesema amechukuwa maamuzi hayo kutokana na sababu tatu ikiwemo ukiukwaji wa maamuzi pamoja na Ubinafsi usiofuata Katiba.

Sababu zingine ni kukosekana kwa uendeshaji mzuri wa Chama nje ya matakwa ya kikatiba, kanuni na taratibu, huku akitaja ubinafsi na umimi na jeuri zilizotawala kwa baadhi ya viongozi wanaotaka kusikilizwa wao pekee huku Mhe Barwany akiongoza kwa uvunjaji wa Katiba.

Katibu huyo kabla ya kuacha ukatibu, alikuwa na nyazifa mbalimbali zikiwemo za uenyekiti wa tawi la Gulf na mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa, na mjumbe wa mkutano mkuu wa kata ya Makonde.

"Nikiwa na akili timamu na bila ya kushawishiwa na kwa kufuata katiba ya Chama, kwa hiyari yangu nimeamua kujiondoa katika nyazifa zote za uongozi ndani ya Chama kuanzia mei 20 mwaka huu uongozi ambao nimedumu nao kwa miaka 15"Alisema Taher.

Aidha,akasema kwa sasa anaendelea kuwa mwanachama wa kawaida, sanjari na kutekeleza matakwa ya kikatiba ya Chama chao na atakuwa mstari wa mbele kufikia malengo ya Chama chao wakati wowote.

Aidha Taher ametoa mfano wa ukiukwaji huo ni pamoja na Kumvua Uanachama Kinyume na Utaratibu Diwani wa kata ya Makonde Manispaa ya Lindi, Abdallah Khatau huku akijua kuwa kwa Mujibu wa katiba Barwany na kamati ya Utendaji haina mamlaka hayo ya kumvua uanachama kiongozi alieteuliwa kuwaongoza wananchi baada ya kupigiwa kura.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top