Diego Costa (kushoto) akishangilia na Koke baada ya kufunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti.
Fernando Torres (kulia) na Samuel Eto'o wakiwa hawaamini kilichowasibu. Kushoto ni Ramires.
Mourinho akipeana mkono na Diego Simeone baada ya kipenga cha mwisho.
Atletico Madrid imetinga Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Chelsea kwa mabao 3-1 kwenye mechi ya Nusu Fainali iliyopigwa Stamford Bridge jijini London usiku wa jana.
Mabao ya Atletico Madrid yamewekwa kimiani na Adrian dakika ya 44, Diego Costa dakika ya 60 kwa penalti na Turan dakika ya 72 wakati bao pekee la Chelsea likifungwa na Torres dakika ya 36 ya mchezo.
VIKOSI:
Chelsea: Schwarzer, Ivanovic, Cole (Eto'o 54), Luiz, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Torres (Ba 67), Willian (Schurrle 77), Hazard.
Waliokuwa benchi: Oscar, Van Ginkel, Kalas, Hilario.
Atletico Madrid: Courtois, Juanfran, Luis, Tiago, Miranda, Godin, Turan (Rodriguez 84), Suarez, Adrian (Raul Garcia 66), Costa (Sosa 76), Koke.
Waliokuwa benchi: Aranzubia. Villa, Alderweireld, Diego.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.