Unknown Unknown Author
Title: AZAMTV YAJA NA KWETU HOUSE (search for the Ultimate Fun)
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
CEO wa AzamTV Rhys Torrington (Kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya Uzinduzi wa Kipindi cha KWETU HOUSE Timu ya KWETU HOUSE Kutoka kushot...
CEO wa AzamTV Rhys Torrington (Kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya Uzinduzi wa Kipindi cha KWETU HOUSE
Timu ya KWETU HOUSE Kutoka kushoto Joseph Mtatiro, Wasiwasi Mwabulambo, Hellen Hartman, Irada Mahadhi na Efe Etiyio
Project Manager wa KWETU HOUSE Wasiwasi Mwabulambo akitoa msisitizo juu ya Kipindi cha KWETU HOUSE
Kwetu House

AzamTV leo wamezindua mashindano yatakayowahusisha wapenzi wa kandanda yatakayojulikana kama KWETU HOUSE. Mashindano haya ambayo ni mara ya kwanza Tanzania yatashirikisha wapenzi na mashabiki wa mpira wa miguu ambapo watu kumi wa 10 wa timu mbalimbali watachaguliwa na kuishi katika nyumba moja kwa muda wa siku 3 wakionyesha ni jinsi gani wao ni mashabiki namba mmoja kwa timu zao .

Akizindua mashindano hayo, Mkurugenzi mtendaji wa AzamTV, bwana Rhys Torrington alisema: "Lengo kuu la kufanya shindano hili ni kuamsha hisia za mashabiki wa soka na kuonyesha umuhimu wa kuthamini mashabiki kwa sababu bila wao mpira wa miguu usingekuwepo leo hii; wakati huo huo ni kuwaletea watazamaji vipindi vinavyoburudisha na kuelimisha".

"Mashindano haya yametokana na ubunifu wa wafanyakazi wa Azamtv ambapo hiki ni kipindi kimojawapo kitakachofuatiwa na vingine vingi ambavyo viko ndani ya maandalizi kupitia kampuni ya Uhai Production ambayo ni kampuni mama ya AzamTV", aliongeza bwana Wasiwasi Mwabulambo ambaye ni mratibu wa mashindano hayo.


Wanaoruhusiwa kushiriki mashindano haya ni wanaume wenye umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.

Wakiwa ndani ya jumba la KWETU HOUSE washiriki wataenguliwa kila siku ya jumapili mpaka kubakia washiriki watatu ambapo mmoja wao atajinyakulia kitita cha shilingi milioni kumi (10).

Usaili wa shindano hili utafanyika siku ya jumamosi tarehe 24/05/2014 uwanja wa Leaders club, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni. Usaili utakuwa ni bure. Pia mashabiki wanaweza kujisajili kwa kutuma video zao fupi kwenda kwenye whatsApp number 0759 38 65 68 nakuonyesha ushabiki wao wa dhati.

Watakaochaguliwa watatangazwa tarehe 27/05/2014 ambapo wataingia ndani ya jumba la KWETU HOUSE tarehe 30/05/2014; na mshindi atapatikana tarehe 27/06/2014.


Shindano hili limedhaminiwa na Azam Energy Drink kwa ushirikiano wa Channel Ten, Magic Fm na Times Fm.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top