Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Boniface Wambura akizungumza na vyombo vya habari.
OFISA Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Boniface Wambura akizungumzia kuhusiana na mapato yaliyotokana na mechi kati ya Taifa Stars na Zimbabwe iliyochezwa wiki iliyopita ambapo jumla ya shilingi milioni 63 zilipatikana baada ya mashabiki elfu kumi na moja kujitokeza kuangalia mchezo huo.
Pia alizungumzia kuhusu siku ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo itaanza kuchezwa Agosti 24 mwaka huu ambapo ligi hiyo itahusisha timu 14 na tiketi za eletroniki zitatumika.
Pia kurudi kambini kwa timu ya Taifa Stars kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Zimbabwe mchezo utaopigwa Juni mosi mwaka huu jijini Harare, Zimbabwe. Pia TFF wameandaa safari ya mashabiki watakaohitaji kwenda na timu nchini humo kwa kuchangia gharama ya shilingi laki tatu kwenda na kurudi.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.