Unknown Unknown Author
Title: MKASA::: UNAAMBIWA KUWA HARAKA NA UBUSY HAUFAI...HEBU SOMA KISA HICHI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Miaka 10 iliyopita kijana mmoja aliyekuwa akifanya kazi kama mkurugenzi wa kampuni mmoja mashuhuri alikuwa akisafiri kwa gari kutoka mji m...
Gari
Miaka 10 iliyopita kijana mmoja aliyekuwa akifanya kazi kama mkurugenzi wa kampuni mmoja mashuhuri alikuwa akisafiri kwa gari kutoka mji mmoja kwenda mwingine.
Gari lilikuwa spidi sana na wakati huo alikuwa akiwangalia baadhi ya watoto waliokuwa wakicheza na akapunguza mwendo kwani alihisi kuna kitu amekiona kabala ya kushtushwa na kipade cha tofali kilichorushwa na kuupiga mlango wa gari lake jipya na la gharama ambalo lilikuwa na miezi miwili tangu anunue..

Akasimama haraka na kuliangalia gari lake nakuona limechubuka rangi na mlango kubonyea na akamwona mtoto aliyelirusha lile tofali na kwa sura ya ukali akamsogelea na kumwambia unajua ulichokifanya kitakugharimu kiasi gani wewe na familia yako??
Yule mtoto akawa akilia na kumwomba samahani yule kijana huku akisema nilirusha tofali lile ili nipate msaada kwani nimekaa kwa muda na kila nikiomba msaada watu kusimama hakuna aliyefanya hivyo.
Huku machozi yakimtoka akamwonyesha yule kijana nyuma ya gari moja lililopaki na kuona kuna kijana mmoja mlemavu kaanguka kutoka katika kiti chake cha kutembelea baada ya kiti kuteleza na kisha kuanguka na mdogo akashindwa kumrudisha.
Yule kijana huku akijikaza kujizuia hasira na kuvuta pumzi nzito na kushusha kwa mfululizo akamsaidia yule mlemavu kurudi kwenye kiti na akatoa kitambaa chake na kujifuta vumbi huku akangalia yule mdogo akamsukuma kaka yake katika kile kiti na kutokomea kuelekea kwao..
Akalifuata gari lake na kuondoka kuendelea na safari huku akiwaza jinsi yule mtoto alivyoamua kuchukua ujasiri ule kuokoa maisha ya kaka yake na kuona jinsi wanadamu tunavyosongwa na mambo yetu na kusahau kuwa kuna watu wanahitaji msaada wetu kwa jinsi yule mtoto alivyojaribu kusimamisha watu bila mafanikio.
Kijana yule hakulitengeneza lile eneo ambako kile kipande cha tofali kilipiga ili iwe kama sehemu ya kumkumbusha kuwa hatakiwi kuwa na haraka katika maisha au busy na maisha mpaka mtu amrushie kipande cha tofali ili kipata masaada wake au kumkumbusha kuwa alihitaji msaada wake.
Kuna vipande vingi vya tofali katika maisha yetu, vingine vikubwa na vingine vidogo ambavyo kila siku tukutana navyo bila kujua au kwa kujua na kupuuzia.
Kamwe usiwe busy na maisha na kuja kukumbuka kuwa kuna nyakati nyingi za furaha na faraja uliziacha njiani au hata kupoteza watu muhimu kwa kuwa wao hawakukurushia tofali ili kukukumbusha kuwa uwepo wako kwao unahitajika.
Mungu atujalie wepesi wa mapito yetu na busara tele
Comment AMEN na kisha share na kisha Mungu akujalie hekima na busara katika maisha yako

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top