Afisa Huduma kwa Wateja wa Tigo,Deo Rupia (kulia) akikabidhi zawadi kwa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi,Kelvin Makonda mara baada ya mkuu huyo
kuzindua kituo cha Huduma kwa Wateja cha Tigo, Lindi Manispaa
Mkurugenzi Manispaa ya Lindi,Kelvin Makonda akikata utepe kuzindua rasmi
kituo cha huduma kwa wateja cha Tigo ambacho kitatoa Huduma kwa wateja wa
mkoa huo ili kurahisha huduma za kampuni Hiyo
Tawi jipya la kampuni ya Tigo Mjini Lindi lilizinduliwa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi,Kelvin Makonda akiwa katika Picha ya pamoja
na wafanyakazi na mawakala wa kampuni hiyo
Akikagua sehemu mbalimbali za utoaji huduma baada ya kuzindua tawi hilo.
Na Abdulaziz Lindi
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo leo imezindua tawi jipya la huduma kwa wateja mkoa wa Lindi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zake kwa mkoa huo ili wateja wapate huduma za moja kwa moja toka kwa kampuni hiyo.
Akizindua ofisi hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi, Kelvin Makonda ameipongeza kampuni hiyo kwa hatua hiyo ya kusogeza huduma kwa jamii zilizopo mikoa na wilaya za pembezoni kwa kupata huduma za mawasiliano zitolewazo na kampuni hiyo ikiwemo kupiga simu, kurejesha namba iliyopotea,Usajili,mtandao wa Intaneti pamoja na huduma za kibenki kwa urahisi elimu ya rahisi ya matumizi ya mtandao kwa simu zenye uwezo mkubwa (smartphones) na kuiweka jamii katika Dunia ya sasa, alimalizia Makonda
Aidha alieleza kuwa kuwepo kwa ofisi hiyo mjini Lindi kutachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi ikiwemo Manispaa yake kuongeza pato kwa kodi mbalimbali zitakazolipwa na Kampuni hiyo ambapo pia matarajio ya wengi wanategemea kuwa kampuni hiyo itaongeza uchangiaji wa huduma za kijamii pamoja na utatuzi wa kero za mawasiliano naamini kuwa Duka hili litakuwa kama Kituo muhimu cha kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wa mtandao huo na tunategemea sasa kutasaidia pia wateja wake kupata
Nae Afisa Mahusiano wa Tigo Bi Pilila Kavishe ameeleza kuwa Tawi hilo linatarajia kuhudumia wateja wengi kwa siku na kuleta manufaa makubwa kwa wakazi wa wilaya za Ruangwa, Liwale, Nachingwea ambapo pia zitauzwa simu za aina mbalimbali kwa bei nafuu.
Kuzinduliwa kwa Tawi hilo limefanya kampuni hiyo kuwa na Maduka 41 ambayo yamesogeza huduma kwa jamii katika mikoa yote Nchini.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.