Na.Paul Manjale
Kuelekea tuzo za mwanasoka bora Epl (PFA) jumapili hii kiungo Aaron Ramsey anayekipiga na klabu ya Arsenal ametoboa siri juu ya nani hasa ndiye chaguo lake katika kinyang'anyiro hicho.
Ramsey ambaye amekuwa na msimu mzuri na kufanikiwa kufunga magoli tisa licha ya kuwa nje kwa miezi minne kutokana na majeruhi ya misuli amesema kura yake ameitoa kwa mshambuliaji wa klabu ya Liverpool mruguay Luis Suarez ambaye mpaka sasa ameshafumania nyavu mara 30 katika michezo 30 ya ligi kuu.
Pia Ramsey ameonyesha waziwazi kuwatabiria ushindi washindani wake Eden Hazard na Daniel Sturridge katika tuzo ya mchezaji bora kijana (Chipukizi) mbele ya Luke Shaw, Raheem Sterling, Ross Backley na yeye mwenyewe na kusema kuwa nyota hao wanastahili kutokana na ubora waliouonyesha mpaka sasa.
Ramsey ameongeza kitendo cha yeye kuwa ni mmoja kati ya watu wanaogombea tuzo hiyo ni heshima kubwa na ameridhika vya kutosha kwani malengo aliyojiwekea kabla ya msimu yametimia.
Tags
SPORTS NEWS
