Unknown Unknown Author
Title: MAHABA:: ASICHOKIPENDA MPENZI WAKO, KUNA HAJA GANI KUKILAZIMISHA?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
NI matumaini yangu kuwa umzima unaendelea vyema na majukumu ya kila siku kama kawaida. Mpenzi msomaji, hakuna kitu kizuri kama wapenzi walio...

NI matumaini yangu kuwa umzima unaendelea vyema na majukumu ya kila siku kama kawaida. Mpenzi msomaji, hakuna kitu kizuri kama wapenzi waliotokea kupendana kwa dhati kuridhiana katika kila jambo.mahaba 1Tufahamu kwamba kutofautiana katika mambo ambayo yanagusa maisha hasa kwa wanandoa ni tatizo linaloweza kusababisha nyufa na furaha kutoweka.

Mara kwa mara nimekuwa nikizungumza na watu walio kwenye ndoa, wengi wanaeleza kuwa kuna wakati hujikuta wakisuguana katika mambo kadha wa kadha ambayo huwafanya wanuniane au wengine kufikia hatua ya kupigana.

Ndiyo maana kuna wakati najiuliza, kama umebaini kitu f’lani mwenza wako hakipendi na kuna uwezekano wa kukiacha na maisha yenu yakaendelea kuwepo, kuna haja gani kukilazimisha? Sioni kama kuna haja ya kukilazimisha kwa sababu mwishoni mtagombana na kuifanya amani itoweke.

Yapo mambo mengi ambayo wapenzi na wanandoa wamekuwa wakilazimishana. Mmoja anataka mwingine hataki na hatimaye kutokea hali ya kutoelewana.

Leo nimeona nizungumzie machache ambayo kama unataka uhusiano wako uwe salama, inapotokea mpenzi wako amesema hataki huku akitoa sababu za msingi, wewe usilazimishe, kubaliana naye.

mahaba 2Mapenzi
Nimeshawahi kusema huko nyuma kwamba, mapenzi ni suala la kuridhiana kwa wawili waliotokea kupendana. Kila mmoja kuna wakati anatamani kufanya tendo hili lakini si kila utakapojisikia basi na mwenza wako atakuwa anajisikia.

Utakuta wanandoa mara kwa mara wanatofautiana katika jambo fulani mwishowe wanagombana. Iko hivi, kama mkeo anakuambia hajisikii kufanya tendo hilo kwa wakati f’lani kutokana na sababu za msingi, ya nini wewe ulazimishe na kuanza kutoa maneno yasiyo mazuri?
Kwa nini wewe mwanamke mumeo anapokuambia hajisikii wewe ukimbilie kudai anatoka nyumba dogo? Tusilazimishane, tujue furaha katika tendo hili inapatikana kwa wawili kuridhiana.

Mtoto
Wapo baadhi ya wanaume huwa nawashangaa sana. Unakuta kaanzisha uhusiano na msichana huku akimweleza kuwa anampenda sana na ana malengo ya kufunga naye ndoa lakini baada ya muda anaanza kulazimisha yule mpenzi wake amzalie kwanza mtoto ndipo ndoa ifungwe.
Hivi hapo kuna busara kweli? Cha ajabu mwanaume huyo akikataliwa katika hilo, anasitisha uhusiano au anapunguza mapenzi.

Achilia mbali wanaoingia kwenye ndoa, wapo wanandoa ambao hutofautiana katika suala la kutafuta mtoto aidha wa kwanza au mwingine. Baadhi ya wanawake hawapendi kuzaa watoto wengi. Wakizaa wawili tu, hawataki tena.

Lakini wakati wao wakiwa na uamuzi huo, waume zao wanataka kuwa na watoto wengi.

Matokeo yake sasa msuguano unatokea, huyu anataka mtoto, yule hataki. Mimi nadhani katika hili ni suala la watu kukaa na kushauriana na kufikia muafaka.

Anayetaka mtoto atoe sababu zake na asiyetaka mtoto naye aseme kwa nini. Mmoja lazima atakuwa na sababu za msingi na kwa ushawishi wake anaweza kuweka mambo sawa.

Mavazi
Mke wa mtu hakika anatakiwa kuvaa kiheshima, hilo halina mjadala. Anatakiwa kujifikiria mara anavaa nini anapokwenda wapi. Wanaume wengi wamekuwa wakikorofishana na wake zao kutokana na suala la mavazi.

Katika hili naomba niseme kwamba, kama mumeo hataki uvae nguo f’lani, huna sababu ya kulazimisha. Utakapolazimisha utaonesha kumdharau na kwamba huenda kuna mtu mwingine unamvalia, jambo ambalo si zuri hata kidogo.

Hata wewe mwanamke, huenda kuna nguo ambazo mumeo akivaa hupendi, mwambie! Naamini kukubaliana katika hilo kutaepusha mikwaruzano isiyo ya lazima.

Marafiki
Yawezekana kuna aina ya watu ambao mumeo/mkeo au hata mpenzi wako hapendi kukuona nao. Kama kweli unajali uhusiano wako, kuna haja gani kulazimisha kuwa nao karibu? Wao watakusaidia nini?
Kumbuka kila kukicha unachotakiwa kukifanyia kazi ni kuangalia yapi yataboresha uhusiano wako na yapi yatabomoa.
Marafiki wasiofaa, waweke pembeni na wale unaowaona wana faida kwenu na mwenza wako naye anawakubali, wakumbatie.

Kuchelewa kurudi nyumbani
Kama wewe ni mtu unayeijali familia yako, ni lazima utakuwa unaimisi unapokuwa mbali nayo. Pia kwa mume anayempenda na kumthamini mke wake, akiwa mbali naye lazima atakuwa anaumia.

Kama wewe unafanya kazi na mchana kutwa unakuwa mbali na mwenza wako, unapotoka kazini kuna ulazima gani wa kupitia baa au vijiweni kwa marafiki kisha kurudi nyumbani usiku?

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top