Mwanafunzi:’huenda hii ndio mara yangu ya mwisho kukuambia kuwa nakupenda,’ndio ulikuwa ujumbe wa mwanafunzi mmoja kwa jina Shin Young-Jin kwa mamake.
Mama:”na mimi nakupenda mwanangu,” alijibu mama yake Shin kwa ujumbe wa simu bila kujua kilichokuwa kinaendelea.
Kulingana na jarida la Herald nchini humo, Shin alikuwa miongoni mwa watu 179 waliookolewa lakini wazazi wengine waliopokea ujumbe kama huo bado hawajaweza kuwaona watoto wao.
Mawasiliano mengine kati ya mwanafunzi mmoja na babake , yalinukuliwa na shirika la habari la AFP ni haya hapa chini
Mwanafunzi: “baba usijali,nimevaa boya la kujiokoa na niko na wasichana wenzangu. Tuko ndani ya meli na bado hatujaanza kuokolewa.”
Baba: Najua msaada uko njiani,lakini kwa nini hamjaanza kuelea, tafadhali jaribu kuondoka ndani ya meli kama unaweza.”
Mwanafunzi: ”Kuna msongamano mkubwa na meli tayari imeanza kuzama”
Mwanafunzi aliyetuma ujumbe huu bado hajapatikana.
Familia za abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo walijawa na hisia wakisubiri taarifa zozote kuhusu wapendwa wao.
Katika ujumbe mwingine wa simu, mwanafuzni mmoja alimtumia ujumbe kakake mkubwa meli ilipoanza kuzama.
Mwanafunzi: “meli imekwama na haisongi walinzi wa baharini wameanza kuwasili kujua hitilafu imetokana na nini’
Kakake:” usiwe na wasiwasi fanya kila mnachoamrishwa kufanya na kila kitu kitakuwa shwari
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.