UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI WAKAMILIKA ASILIMIA 45

Daraja la Kigamboni limekamilika kwa zaidi ya asilimia arobaini na tano na matumaini makubwa ya kumalizika kwa ujenzi huo kwa muda uliopangwa Julai mwakani yakionekana huku nyumba zilizokuwa zinazuia ujenzi huo zikibomolewa kwa nguvu na serikali.clip_image001Akizungumza jijini Dar es Salaam meneja mradi huo injinia Karim Mattaka amesema ujenzi huo umeshaanza kuleta matumaini makubwa kutokana na nguzo mbili zilizokuwa zinakwamisha kuwa tayari na zoezi linaloendelea ni kuhamisha maji katika maeneo yaliyochimbiwa nguzo hizo sambamba na kuchimbia nguzo kubwa za kupokea Daraja hilo upande wa barabara ya Mandela.

Aidha injinia Karimu amejaribu kufafanua mfumo wa barabara na daraja hilo namna utakavyotumika baada ya kukamilika na kuwahakikishia watanzania ujenzi huo utakamilika kwa wakati kama mambo yataenda kama yalivyopangwa.

Mwenyekiti serikali ya mtaa wa Vijibweni Bw. Athman Ally aelezea kuhusiana na hatua iliyochukuliwa na serikali ya kuvunja nyumba za baadhi ya wakazi waliogomea fidia amesema wao walipewa taarifa na mwanasheria mkuu na baadaye akatakiwa kwenda kusimamia zoezi la uvunjaji wa nyumba hizo.

>>>itv

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post