NDANDA FC YAPATA TSH MILION 22.5, KUMALIZA MCHEZO WAO NA POLISI YA DAR - KARUME

DSC_0119Ofisa habari na mawasiliano wa MTWAREFA ndugu Marino Kawishe

Chama cha soka mkoani mtwara MTWAREFA Kimetoa pongezi za dhati kwa mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simba Kalia kwa jitihada alizofanya za kupatikana kiasi cha Tsh milion 22.5 kwa ajili ya kuisaidia timu ya Ndanda fc katika mchezo wake wa mwisho na Polisi ya dar.

Akizungumza na blog hii m/kti wa chama cha soka Mkoani Mtwara Athuman Kambi amesema fedha hizo zitaaisaidia ndanda fc kulipa madeni pamoja na hotel na vitu vingine ikiwemo posho kwa wachezaji wa timu hiyo kabla ya mchezo wao wao siku ya jumatatu march 24 kwenye uwanja wa Karume dar.

Sanjari na hilo mashabiki wa soka wametakiwa kubeba mabango pekee yakushangilia timu ya Ndanda fc na yakiwa na ujumbe wa kushangalia tu na sio vinginevyo katika mchezo huo.

“tunajua  na tunathamini sana mchango wa ushangiliaji wa mashabiki wa ndanda ila tunachowaomba nikubeba mabango yenye ujumbe wakushangilia ndanda fc na sio vinginevyo” amesema Kambi.

Ofisa habari na Mawasiliano

Chama cha soka Mkoni Mtwara MTWAREFA

Marino kawishe. 0713 984439.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post