NDANDA FC YAFANIKIWA KUPANDA DARAJA NA KUCHEZA LIGI KUU TANZANIA BARA MWAKANI

NDANDA FCHatimae Timu ya Soka ya Ndanda Fc imepanda daraja na Kuingia Ligi kuu Tanzania Bara Baada ya Kushinda Mchezo wao wa Mwisho uliochezwa leo katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam dhidi ya Polisi nayo Africa Lyon imetoa sare na Green wories.
Timu hiyo ya Ndanda Fc imepata Ushindi wa Magoli 2 – 1 katika mchezo huo uliochezwa leo uwanja wa Karume jijini dar es salaam Huku magoli ya Ndanda Fc yakifungwa na Amri Msumi Matokeo hayo ni faraja kwa wakazi wa Mkoa wa Mtwara ambao walikuwa wakiomba Timu yao ya Ndanda Fc iweze kushinda na Kupanda daraja na Kuweza kucheza Ligi kuu Tanzania Bara kwa Msimu ujao na Dua zao zimekubalika kwani Matokeo ya Africa Lyon na Green Wories imeifanya Timu ya Ndanda kuibuka Kidedea.
Hongereni Ndanda Fc

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post