Unknown Unknown Author
Title: RONALDO KUNGOJA RUNGU KUTOKA KWA CHAMA CHA SOKA SPAIN, BAADA YA KUMTOLEA SHUTMA REFA KUIPENDELEA BARCELONA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Cristiano Ronaldo amezungumza baada ya kipigo cha jana kutoka FC Barcelona akisema walikuwa wakicheza Barca yenye wachezaji 12. Mwanasoka hu...

Cristiano Ronaldo amezungumza baada ya kipigo cha jana kutoka FC Barcelona akisema walikuwa wakicheza Barca yenye wachezaji 12.clip_image001Mwanasoka huyo bora wa dunia amesema kwamba refa wa mchezo huo Undiano Mallenco alichangia timu yake kupoteza wa El Clasico hapo jana usiku katika dimba la Santiago Bernabeu.

Madrid walipewa penati ya utata muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza, lakini Mallenco aliwapa Barca penati mbili muda mfupi baadae — pia alimtoa kwa kadi nyekundu Sergio Ramos – na Ronaldo anasema anahisi refa alikuwa akiwapendelea Barcelona kwa makusudi.

“Undiano Mallenco hafai kuchezesha michezo ya namna hii. Tulikuwa tunacheza dhidi ya wachezaji 11 na mwingine wa ziada. Mara zote imekuwa hivi. Ni kama vile hawataki tushinde ili Barca watetee taji la La Liga,” Ronaldo aliwaambia waandishi wa habari.

“Sitafuti visingizio, lakini sitaki kukaa kimya kuhusu hili. Refa huyu hakustahili kuchezesha mchezo wa namna hii.

“Nimekuwa hapa kwa muda mrefu – miaka mitano, nafahamu mambo yanavyoenda. Kama Barcelona wangepoteza mchezo hu, wasingekuwa na matumaini ya ubingwa tena. Sijawahi kuona Madrid wakipendelewa na refa.”

“Pamoja na yote yaliyotokea, Madrid bado tutachukua ubingwa wa La Liga.”

REFA HUYO WA KIHISPANIA amewasilisha maoni ya mchezo huo katika body ambayo yenyewe ndio itatoa uamuzi kama watamuadhibu au la.

MSIKILIZE HAPA:

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top