Na. Mwanja Ibadi, Kilwa
Moto umeteketeza nyumba anayoishi mkuu wa wilaya ya Kilwa,
mkoani Lindi, Abdallah Ulega na kusababisha hasara ambayo idadi yake haijaweza kufahamika hadi sasa.Habari kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na Katibu tawala wa mkoa wa Lindi Abdala Chikota alisema kwamba moto huo, umeweza kuteketeza vifaa mbalimbali vilivyomo ndani ya nyumba ya kiongozi huyo.
Chikota alisema moto umeteketeza nyumba hiyo vikiwemo baadhi ya
vifaa mbalimbali vilivyomo ndani yake, umesababisha hasara kubwa,
ambayo idadi yake bado haijaweza kufahamika mara moja.
Alisema kufuatia tukio hilo ofisi ya mkuu wa mkoa imetoa fedha
Shilingi laki tano 500,000.00 pamoja na chakula kama mchele, uga sukari, mafuta ya kula pamoja na maharage ili kumsaidia mkuu huyo katika kipindi hichi cha majonzi wakati ofisi ikifanya utaratibu mwingine wa kutatua tatizo la makazi yake.Kwa upande wake mkuu wa wilaya Kliwa Abada Ulega alisema kuwa vitu vichache tu ndiyo vimeweza kuokolewa kuwa ni vile ambavyo vilikuwa rahisi kuchukuliwa ikiweno begi la nguo na nyaraka zake na kwamba kwa sasa atalazimika kuishi jengo la Hostel.
Aidha Ulega alisema juhudi za wananchi zimesaidia kuokoa vitu
vichache tu ambavyo ni seti ya makochi, magodolo matatu na kitanda kimoja cha mbao na kwamba tukio hilo la moto limeteketeza nyumba hiyo, familia yake akiwemo mke wake alikuwa safarini na amerejea leo mchana.Kwa upande wake kamanda wa polisi Regnal Mzinga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi unafanyika ili kubaini chanzo cha moto huo.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.