Unknown Unknown Author
Title: MAN CITY YAITUNGUA MAN UNITED, ARSENAL YASHIKWA NA SWANSEA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Manchester City imezidi kuongeza kasi ya kuukimbilia ubingwa, lakini ikaongeza kujenga heshima baada ya kuwachapa watani wao Manchester Unit...

Manchester City imezidi kuongeza kasi ya kuukimbilia ubingwa, lakini ikaongeza kujenga heshima baada ya kuwachapa watani wao Manchester United kwa mabao 3-0.MAN U V MAN CKatika mechi hiyo ya Ligi Kuu England iliyomalizika punde, Eden Dzeko alifunga mabao yote mawili ya City.

Bao la kwanza katika dakika ya kwanza tu baada ya mabeki wa United kuzubaa naye akamalizia kiulainiii.

Pamoja na kujitutuma, Dzeko alifunga bao la pili katika dakika ya 56 baada ya Fellaini na Rio Ferdinand kujichanganya wakati wa kuokoa.

Yaya Toure aliyeng'ara naye akapiga bao la tatu kwa shuti kali la kimo cha panya.


SWANSEA VS ARSENAL (2-2)

Swansea wakiwa nyumbani walionyesha wamepania kufanya kweli baada ya kufunga bao katika dakika ya 11.

Lakini Arsenal wakaamka na kusawazisha katika dakika dakika ya 73 kabla ya Olivier Giroud kutupia la pili katika dakika ya 74.

Lakini dakika ya 90, kiungo Flamini alijifunga hivyo kufanya matokeo yawe sare ya 2-2.

NEWCASTLER VS EVERTON (0-3)

Everton nayo ikaendelea kuchanja mbuga, licha ya kuwa ugenini ikashinda kwa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wake Newcastle.

Wafungaji ni Ross Barkley katika dakika ya 22 na Romelu Lukaku katika dakika ya 52.

Leon Osman naye akafunga bao la tatu zikia zimebaki dakika mbili tu kabla ya mpira kwisha.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top