Unknown Unknown Author
Title: DADPS RUANGWA YATOA TREKTA KWA KIJIJI KATIKA KUENDELEZA KILIMO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Akisaini mikataba ya makabidhiano ya Trekta lililonunuliwa kupitia miradi ya DADPS h...

trekta (1)Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Akisaini mikataba ya makabidhiano ya Trekta lililonunuliwa kupitia miradi ya DADPS huku Mwenyekiti wa kijiji cha Kilimahewa,Bw Ally Seif Malongola akisubiri kusaini mkataba huo,trekta (2)Trekta lililokabidhiwa kwa kijiji cha kilimahewa wilayani Ruangwatrekta (3)Afisa Mtendaji wa kijiji cha kilimahewa, Bw Rajab Mohamed akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi kabla ya kukabidhiwa kwa Trekta, Kutoka kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Ruangwa, Silvanus Kilowoko na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
Reubern Mfune
trekta (4)Katibu Tawala wilaya ya Ruangwa Silvanus Kilowoko akikabidhi Mikataba ya Trekta iliyonunuliwa na DADPS kwa Mwenyekiti wa
Kijiji cha Kilimahewa Ruangwa

Na Abdulaziz ,Ruangwa
Wilaya ya Raungwa katika kutekeleza mpango wa kilimo kwanza
Inahakikisha wakulima wanapata mbegu na zana bora za kilimo ikiwemo matrekta kwa wakati sambamba na kuwawezesha wataalam wa kilimo kutembelea wakulima mara kwa mara kwa lengo la kutoa ushauri ili kuboresha kilimo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Ruangwa, Reubern Mfune katika hafla fupi ya kukabidhi trekta kwa kikundi cha wakulima wa kijiji cha Kilimahewa kata ya Nachingwea wilayani humo.

Mfune aliwataka wananchi kuthamini na kutunza huduma za kijamii
zinazotolewa katika maeneo yao zikiwa ni matunda ya utekelezaji wa
mipango ya serikali ya kuwahudumia wananchi wake katika sekta ya elimu Afya, maji na Kilimo.

Akisoma taarifa fupi ya Halmashauri kwa Mgeni rasmi ambae Pia ni
Katibu tawala Wilaya ya Ruangwa,Silvanus Kilowoko, Mfune alibainisha kuwa kupitia mradi wa DADPS Serikali imetoa fedha jumla ya shilingi milioni 40 na wananchi wamechangia shilingi milioni 4.6 kwa ajili ya kununulia trakta lenye thamani ya shs milioni 43.9 kwa lengo la kutekeleza mpango wa kilimo kwanza na halmashauri ya wilaya Ruangwa imechangia shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya kusafirisha trekta hilo lililonunuliwa Suma Jkt.

"KWA Kuwa dhamira ya serikali wakati wote ni kupeleka huduma za kijamii karibu na wananchi kama tulivyofanya kwa wananchi wa kata hii hivyo basi nawaomba jamii kutoa Ushirikiano kwa halmashauri na kujitolea kuchangia maendeleo na kutumia fursa hii kulima kilimo cha kisasa kwa kutumia mbegu bora na elimu itolewayo na wataalam wa kilimo"Alimalizia Mfune Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya RUANGWA.

Kwa Upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji hicho bw Rajab Mohamed kwa niaba ya wananchi alitoa shukrani kwa serikali na kutoa wito wa
kuongezewa wataalamu wa kilimo ikiwemo upatikanaji wa pembejeo kwa bei nafuu ili kulima kilimo cha kisasa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top