BODA BODA FC LINDI WAFANYA ZIARA YA UJIRANI MWEMA MKOA WA MTWARA

DSC_0539Shamra Shamra ya Madereva Bodaboda wakiwa tayari kuanza safari yao kuelekea Mtwara kucheza Mechi ya Kirafiki na Madereva wenzao wa Eneo la Bima Mtwara.DSC_0545Bendera yao hiyo tayari kwa safari hiyo ya Ujirani mwema kati ya Bodaboda Fc kutoka Lindi na wale wa eneo la Bima Kutoka Mtwara.DSC_0551Salum Amber akisimamia kwa makini swala la usafiri tayari kabisa kwa kuanza safari ya kuelekea Mtwara.DSC_0553Madereva Boda Boda wakiwa Ndani ya Gari katika Safari ya Mtwara kwenda kucheza Mechi ya Ujirani Mwema na Madereva Bodaboda wa eneo la Bima Mtwara.DSC_0031Bodaboda fc Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja katika mchezo wa leo dhidi ya Bodaboda fc LindiDSC_0034Bodaboda Fc Lindi wakiwa katika picha ya pamoja katika mchezo wao wakirafiki uliofanyika leo dhidi ya wenzao wa Bodaboda Fc mtwara katika kiwanja cha Nangwanda.

NA Mwandishi wetu.

Bodaboda fc kutoka Soko kuu Manispaa ya Lindi imefanya ziara ya ujirani mwema na wenzao wa Mtwara Madereva BodaBoda wa eneo la Bima. Madereva Hao wamefanya ziara hiyo kwa ajili ya kujuana na kufanya michezo mbalimbali hasa Mpira wa Miguu ambao Umechezwa Katika Uwanja wa Nangwanda Mtwara Mjini.

Madereva  Hao wa Mtwara wameonyesha ukarimu wa Hali ya Juu kwani waliweza Kuwapokea wenzao Kutoka Lindi na kuwapa ushirikiano mzuri wa Kutosha kwa kuwafikisha sehemu ya Kupumzikia wakati wa kusubiri Muda wa kufanyika Mchezo huo wa kirafiki.

Kabla ya Mchezo huo waliweza kubadilishana mawazo kuhusiana na changamoto wanazozipata katika kazi yao hiyo na kuweza kukumbushana mambo muhimu yanayowapasa kufanya ili kufuata sheria za Barabarani na kubwa kuheshimu wateja wao wanao wapa huduma hiyo ya usafiri kwa kuwa waaminifu kwao.

Pia waliweza Kuchukua dakika kadhaa kuwaombea wenzao ambao wameweza kutangulia Mbele za haki, kwa kukaa kimya dakika kadhaa kabla ya mchezo kuanza na kufunga vitambaa vyeusi kuonyesha maombolezo.

Mchezo huo ulikuwa ni Mkali kwani Timu zote zilionekana kujiandaa vizuri na Mchezo huo lakini Ni timu kutoka Lindi ndio ilikuwa Yakwanza kupata Goli kupitia Mchambuliaji wake Ndugu Omari Mbalabala kwa kupiga shuti kali langoni mwa wapinzani wao na Mpira huo Kugonga Mtambaa Panya na Kutika wavuni.

Madereva Wa Mtwara walionekana kuja juu mara baada ya Kufungwa Goli hilo na Kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Madereva kutoka Lindi na kuweza Kusawazisha Goli hilo kupitia kwa Mchezaji wao aliyetambulika kwa jina moja tu la Mgombezi kwa kupiga shuti kali na kumuacha Goli kipa akishangaa na asijue nini cha kufanya.

Hadi mwisho wa Mchezo huo Matokeo yalibaki kuwa Bodaboda Fc Mtwara 1 – 1 Bodaboda Fc Lindi.

Hizi ni Picha kile kilichojiri katika Ziara hiyo:

DSC_0556Safari ikiendelea kuelekea Mtwara kwa ajili ya mechi ya Kirafiki kati ya BodaBoda Fc Lindi na wale wa eneo la Bima Mtwara.DSC_0560Hakika walikuwa na Furaha sana Madereva hawa kwani walionyesha Vibweka vya hapa na pale Hapa wakiwa eneo la Mnazi mmoja Lindi wakielekea Mtwara kwa ajili ya Mechi ya Ujirani mwema kati ya Madereva BodaBoda wa Eneo la Bima.DSC_0565

DSC_0579Madereva wakiwa na furaha ya kukutana na wenzao wa Mtwara wakiwa katika Picha ya Pamoja.DSC_0586Viongozi wa Lindi na Mtwara wa Madereva Boda Boda wakipanga namna ya jinsi mambo yatakavyo kuwa katika safari yao hiyo. DSC_0016Ustadhi Khanafi Abdallah Suleiman kutoka Lindi akitoa nasaha kabla ya mchezo kuanzaDSC_0018Madereva Bodaboda wakisikiliza mawaidha yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa msafara na wale wa Mapokezi katika Ziara hiyo ya Ujirani mwema kati ya Mwara Na Lindi.DSC_0027Kiongozi wa BodaBoda Fc Mtwara akitoa neno kabla ya mchezo huo wa kirafiki uliofanyika leo katika uwanja wa Nangwanda Mjini Mtwara. DSC_0019Wakisikiliza Nasaha kutoka kwa kiongozi wa Bodaboda Fc Mtwara kabla ya mchezo wao wa kirafiki.DSC_0021Wachezaji wa BodaBoda Fc kutoka Mtwara wakisikiliza nasaha kutoka kwa Viongozi wao, kabla ya mchezo wa kirafiki na Bodaboda fc kutoka Lindi.DSC_0022Wachezaji wa BodaBoda Fc kutoka Lindi wakisikiliza nasaha kabla ya Mchezo kuanza.DSC_0037Benchi la Ufundi la Bodaboda Fc Lindi wakifuatilia mchezo uliokuwa ukiendelea katika kiwanja cha Nangwanda Mtwara dhidi ya Bodaboda Fc Mtwara.DSC_0039Benchi la Ufundi la Bodaboda Fc Mtwara wakifuatilia mchezo uliokuwa ukiendelea katika kiwanja cha Nangwanda Mtwara dhidi ya Bodaboda Fc LindiDSC_0042Mtanange ulikuwa mzito kwani Timu zote zilionesha umakini wa Hali ya juu.DSC_0045Hili nikati ya Shambulizi Moja la hatari aliloweza kuokoa kipa huyu wa BodaBoda Fc kutoka LindiDSC_0047Heka heka Golini kwa Bodaboda Fc Mtwara na zilizaa Goli moja la kuongoza kupitia Omari Mbalabala Picha ya Chni akishangilia goli Hilo.DSC_0048

DSC_0051Mashabiki wa Bodaboda fc Mtwara wakifuatilia Mpira huo.DSC_0056Bodaboda Fc wakishangilia goli mara baada ya Mchezaji wao Mgombezi kuifungia timu hiyo goli la kushawazisha.DSC_0059Refa akionyesha ujuzi wake katika kuchezea mpiraDSC_0078Viongozi wakipongezana mara baada ya kumaliza mpirahuo uliokuwa na matokeo ya 1 – 1. Nakuweza kuagana na kuanza safari ya kurudi Lindi.DSC_0081

DSC_0087

DSC_0095

DSC_0103

DSC_0106

DSC_0108

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post