WEST HAM imeijulisha FA nia yao ya kukata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu ya Straika wao Andy Carroll aliyopewa Juzi Jumamosi walipoifunga Swansea City.
Carroll alipewa Kadi Nyekundu na Refa Howard Webb baada kugongana na Beki wa Swansea, Chico Flores.West Ham walikuwa na nafasi hadi hii leo Saa 10 Jioni, Bongo Taimu, kuwajulisha FA nia yao kama wanataka kupinga Kadi hiyo na baada kufanya hivyo taratibu zinawapa Masaa mengine 24 ya kutayarisha na kuwasilisha Ushahidi wao kuipinga Kadi Nyekundu hiyo.
Juzi,mara baada ya Mechi, Meneja wa West Ham Sam Allardyce alimlaani Chico Flores kwa kusababisha Andy Carroll atolewe na kudai wataikatia Rufaa Kadi hiyo.
Baada West Ham kukata Rufaa, Jopo Huru la Watu Watatu litakaa na kupitia ushahidi wa pande zote, Marefa na West Ham, na pia kuangalia Mkanda wa Video wa Tukio lenyewe na kisha kutoa uamuzi.
Ikiwa Rufaa itatupwa nje, Carroll atatumikia Kifungo cha Mechi 3 na kuzikosa Mechi za Timu yake dhidi ya Aston Villa, Norwich na Southampton.
Mechi hiyo na Swansea ilikuwa Mechi ya 3 tu kwa Carroll kurudi Uwanjani baada kuwa Majeruhi kwa karibu Miezi 8 na ni yeye ndie alietengeneza Bao zote mbili zilizofungwa na Kevin Nolan walipoichapa Swansea Bao 2-0.
MATA ADAI GUNDU LITAISHA!Mchezaji mpya wa Mabingwa Manchester United, Juan Mata, amedai bahati mbaya iliyowasakama itaisha hivi karibuni.
Juzi Man United walikikwaa kipigo cha 8 kwenye Ligi Kuu England walipofungwa 2-1 na Stoke City huku Robin van Persie, Wayne Rooney na Mata wakianza Mechi ya kwanza pamoja kwa mara ya kwanza.
Lakini Mata anaamini bahati mbaya itaisha na amesema: “Bahati mbaya hatukushinda Mechi yetu ya pili Wiki hiyo. Ni Uwanja mgumu na upepo mkali haukusaidia kucheza Soka. Lakini hatukustahili kufungwa!”
Aliongeza: “Tulikuwa na bahati mbaya kwa Goli lao la kwanza, tukarudisha na tulijua tutashinda lakini tukafungwa la pili kwa Bao la bahati pia. Tulipata nafasi nzuri hatukuzitumia. Lakini tunahisi hatuwezi kufungwa tena Gemu kama hizi. Natumai ile bahati iliyotoweka kwetu itarudi tena kwani tuna bahati mbaya hata kwenye Majeruhi. Tulipoteza Masentahafu wawili kabla Haftaimu. Lakini naamini tutaanza mbio za ushindi na kuwa bora zaidi!”
LIGI KUU ENGLAND RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Februari 8
1545 Liverpool v Arsenal
1800 Aston Villa v West Ham
1800 Chelsea v Newcastle
1800C rystal Palace v West Brom
1800 Norwich v Man City
1800 Southampton v Stoke
1800 Sunderland v Hull
2030 Swansea v Cardiff
Jumapili Februari 9
1630 Tottenham v Everton
1900 Man United v Fulham
Jumanne Februari 11
2245 Cardiff v Aston Villa
2245 Hull v Southampton
2245 West Ham v Norwich
2300 West Brom v Chelsea
Jumatano Februari 12
2245 Arsenal v Man Unitwd
2245 Everton v Crystal Palace
2245 Man City v Sunderland
2245 Newcastle v Tottenham
2245 Stoke v Swansea
2300 Fulham v Liverpool
MSIMAMO:
NA | TIMU | P | GD | PTS |
1 | Arsenal | 24 | 26 | 55 |
2 | Man City | 23 | 42 | 53 |
3 | Chelsea | 23 | 23 | 50 |
4 | Liverpool | 24 | 29 | 47 |
5 | Everton | 24 | 12 | 45 |
6 | Tottenham | 24 | -1 | 44 |
7 | Man Utd | 24 | 10 | 40 |
8 | Newcastle | 24 | 1 | 37 |
9 | Southampton | 24 | 7 | 35 |
10 | Aston Villa | 24 | -7 | 27 |
11 | Stoke | 24 | -14 | 25 |
12 | Swansea | 24 | -6 | 24 |
13 | Hull | 24 | -7 | 24 |
14 | Sunderland | 24 | -11 | 24 |
15 | Norwich | 24 | -18 | 24 |
16 | Crystal Palace | 24 | -18 | 23 |
17 | West Brom | 24 | -6 | 23 |
18 | West Ham | 24 | -9 | 22 |
19 | Cardiff | 24 | -22 | 21 |
20 | Fulham | 24 | -31 | 19 |
CREDIT TO SOKA IN BONGO
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.