Unknown Unknown Author
Title: TATIZO LA UMEME LINDI KUANZA KUONDOKA HIVI KARIBUNI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa Tanesco mkoa wa Lindi Eng John Bandiye Ofisi ya Mkoa Tanesco Lindi Baadhi ya Vifaa vilivyowasili kwa ajili ya kuondoa kero za umem...

meneja wa tanesco lindiMeneja wa Tanesco mkoa wa Lindi Eng John Bandiyeofisi tanescoOfisi ya Mkoa Tanesco LindivifaaBaadhi ya Vifaa vilivyowasili kwa ajili ya kuondoa kero za umeme ikiwa pamoja na kuondoa ukatikaji wa umeme mara kwa mara kwa sababu ya Nguzo kuchakaa na kuanguka mara kwa mara hususan katika njia kuu ya Mtwaravifaa. 2

Na Abdulaziz Video,Lindi
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco)mkoani Lindi,limeanza kupokea vifaa mbalimbali, zikiwemo nguzo, Mita na waya, vitakavyotumika kuwaunganishia wateja wapya wapatao 1,413 waliokwishaomba kupatiwa huduma hiyo na kulipia kati ya June na Disemba 2013.

Meneja wa Shirika hilo mkoani Lindi, Eng John Bandiye ameyaeleza hayo jana alipokuwa akizungumza na timu ya waandishi wa Habari kuhusiana na jitihada za shirika kutoa huduma kwa wateja.

Vifaa hivyo vimeanza kuwasili mkoani hapa, kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu, na tayari vimeanza kugaiwa Katika wilaya zote tano zilizopo katika mkoa huo.

Amevitaja vifaa vilivyowasili kuwa ni pamoja na Mita za LUKU 1,413,
Nguzo 450 kwa ajili ya Service Line katika njia kubwa za umeme na
kwenye mita majumbani.

Meneja Bandiye amefafanua kuwa kufuatia kupatikana kwa vifaa
hivyo, tayari wateja wapatao 1,413 waliotuma maombi ya kupatiwa umeme na kulipia kwa muda mrefu uliopita, wataunganishiwa huduma hiyo katika kipindi kifupi kijacho kuanzia sasa, ili waondokane na tatizo hilo lililodumu kwao kwa muda mrefu.

Aidha ameeleza pia katika maombi 1,413 waliyoyapokea kutoka kwa
wateja wapya mwaka 2013, wapo 1,132 hawahitaji nguzo na 281 ndio
wanaohitaji kupelekewa nguzo na kubainisha kwa kusema wilaya ya Lindi waliotuma maombi yao ni (509) kati ya hao (73) wanaohitaji kupelekewa nguzo, Nachingwea 322 wasiohitaji nguzo ni 263, Kilwa 275 wakiwemo (81) wanaohitaji nguzo, Liwale 154 kati yao 128 hawahitaji nguzo na Ruangwa wapo 153 wanaohitaji huduma ya nguzo ni 42.

"Tatizo kubwa lililochelewesha wateja wetu wakae muda mrefu ilikuwa ni vifaa, kwa vile vimewasili tatizo hilo,naweza kusema limeisha na kazi ya kuwaunganishia wateja wetu limeanza, hivyo hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Februari 2014, zoezi la kuwaunganishia umeme liwe limekamilika" Alisema Bandiye.

Kutokana na kufika kwa vifaa hivyo amewashauri wale wateja wapya ambao walikuwa wakisita kulipia kwa hofu ya kuchelewa kuunganishiwa, wafanye hivyo bila ya kukosa ili na wao waweze kufungiwa Mita kwa lengo la kupatiwa huduma waliyoiomba ambayo pia kwa sasa imepunguzwa bei hadi kufikia 27,000/= kwa wateja walio vijijini kulikopita bomba la Gesi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top