RAYUU AKOMALIA WAUME ZA WATU

MSANII kinda kwenye tasnia ya filamu Bongo, Rahma Bagenzi ‘Rayuu’ amesema kuwa, kamwe hatokoma kutembea na waume za watu kwa kuwa sheria ya dini yake ya Kiislamu inamruhusu kuolewa na mume wa mtu.clip_image002Rahma Bagenzi ‘Rayuu’.

Akipiga stori na paparazi wetu, Rayuu alisema kipindi cha nyuma aliwahi kutoka kimapenzi na mume wa mtu (hakumtaja jina) na kufikia hatua ya kufikishwa polisi na mwenye mke lakini haimaanishi kuwa hatatembea tena na mume wa mtu.
“Nikila kiapo cha kutotembea na waume za watu nitakuwa naongopa, kwanza dini yetu imeruhusu ndoa za uke wenza huenda  Mungu kaniandikia niolewe ndoa ya aina hiyo sina uwezo wa kupingana naye,” alisema Rayuu.

CREDIT: GPL

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post