Unknown Unknown Author
Title: HABARI MUHIMU: MCHEZAJI AFA UWANJANI DODOMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na John Banda, Dodoma MCHEZAJI wa Reli Tabora na Reli Dodoma Masudi Juma amekufa uwanjani baada ya kuanguka kabla ya kuanza mazoezi. Maut...

breaking news

Na John Banda, Dodoma

MCHEZAJI wa Reli Tabora na Reli Dodoma Masudi Juma amekufa uwanjani baada ya kuanguka kabla ya kuanza mazoezi.

Mauti hayo yalimkuta jana baada ya kuanguka katika uwanja wa kilimani alikwenda kufanya mazoezi na timu ya vetelani ya mkoa wa Dodoma

Katibu mwenezi wa vetelelani Dodoma Mussa Kunga alisema tukio hilo lilitokea wakati wakifunga kamba za magoli kwa ajili ya kuanza mazoezi na wakashtuka Marehemu akianguka na kupoteza fahamu na ndipo walipoamua kumkimbiza hospital.

‘’Tulishtuka Maulid alipoanguka hata kabla hatujaanza kufanya mazoezi japo tayali alishazunguka uwanja mara tatu na akawa pembeni akituangalia wakati tukufunga kamba za magoli ndipo alipoanguka wakati tunampeleka hospital akafa njiani’’, alisema Kunga

Aidha Kunga alisema marehemu Maulid Juma alizaliwa mwaka 1958 mkoani tabora alianza kucheza mpira 1980 katika klub ya Reli Tabora na 2000 akahamia Reli Dodoma kabla ya mwaka 2002 kujiunga na Vetelan Dodoma ambapo amekuwepo mpaka mauti inapomkuta.

Mwili wa Marehemu Maulid Juma umesafirishwa jana jioni kwa njia ya Reli kutumi kiberenge ambapo mazishi yanatarajia kufanyika kesho mkoani humo Mungu ailaze mahali pema peponi Amina.

CREDIT : MZEE WA MATUKIODAIMA

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top