Unknown Unknown Author
Title: WEMA NA JOKATE WAMALIZA TOFAUTI ZAO JIJINI ARUSHA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wema Sepetu na Jokate Mwegelo si maadui tena. Uhusiano wa warembo hao ambao mwaka 2006 walishiriki shindano la Miss Tanzania, ambapo Wema ak...

Wema Sepetu na Jokate Mwegelo si maadui tena. Uhusiano wa warembo hao ambao mwaka 2006 walishiriki shindano la Miss Tanzania, ambapo Wema akawa mshindi na Jokate kukamata nafasi ya pili, uliharibika, baada ya Wema kumtuhumu Jokate kumchukulia mpenzi wake, Diamond Platnumz.clip_image001“Mimi na Naseeb tuliachana baada ya yeye kunicheat na Jokate,” Wema aliliambia jarida la Mzuka mwaka jana.

“Siku moja ndio nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi Piccolo akaniambia ‘Diamond yuko hapa na Jokate na wanakiss’. Nilitoka, nikachukua taxi nikaenda mpaka Piccolo, kitu cha kwanza niliona gari yake. Nilivyofika nikawakuta sijui wamewekeana miguu. Nilivyofika pale nikawasalimia wakawa wako kimya na nimeona ile kitu nikawaaga nikaondoka zangu.”

Hata hivyo, mastaa hao wanaonekana kusahau yaliyopita na kuganga yajayo baada ya Jokate kupanda jukwaani kwa surprise jijini Arusha kwenye show ya msanii wa Wema, Mirror na wawili hao kucheza pamoja kuashiria kuwa hakuna tena beef kati yao.

clip_image001[5]Wema na Jokate wakiwa kwenye show ya Mirror jijini Arusha

Hata hivyo kwenye mahojiano aliyofanya na jarida la Vibertz mwaka jana, Jokate alidai kuwa kwa kuanzisha uhusiano na Diamond hakunuia kumuumiza Wema.

“I never intended to hurt anyone, lakini hata hivyo Diamond gave me the impression kwamba Wema alikuwa anamcheat and he wanted to leave her. Sikudhamiria kumuumiza Wema, huo ndio ukweli,” alisema Jokate.

clip_image001[7]Wema na Jokate wakicheza muziki pamoja

clip_image001[9]Uhusiano wa Diamond na Jokate ulidumu kwa miezi miwili tu.

Kwa upande wa Diamond, mwaka jana alikiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV kuwa Jokate ndiye msichana aliyemuumiza zaidi.

“Kwasababu alikuwa too innocent halafu hakuwahi kunikosea kitu chochote Jokate kabisa, halafu nikamwingiza kwenye matatizo, watu wakamchukulia tofauti kwamba ‘Jokate kamchukulia Wema boyfriend wake’ wakati nilimfuata mimi kama mimi, nilimtafuta mwenyewe halafu then nikawa niko naye halafu ghafla nikarudisha mahusiano kwa Wema. Sikujiskia vizuri halafu still haikuwa vizuri so sometimes nikikaaga hivi nasema nilimkosea,” alisema Diamond.

Akijibu swali la kwanini alimuacha Jokate, Diamond alidai, “Sijui nilirogwa hata sijui, I don’t know, sijui hata kwanini, hakuwahi kunikosea chochote sio, sababu nilikuwa nikikaa naye alikuwa akinishauri vitu vingi vya maendeleo, sijui ulikuwa ni utoto sielewi yaani, sijui ni kitu gani, nilijikisa vibaya sana, halafu mtoto wa watu mstaarabu sana, alijitahidi kujenga career yake sasa hivi imekaa vizuri.”

CREDIT: BONGO5

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

  1. Women never solve their conflicts genuinely, especially if the conflicts come to involvement of men..PERIOD.

    ReplyDelete

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top