Unknown Unknown Author
Title: NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO KILWA MASOKO USIKU WA KUAMKIA LEO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Abdulaziz Ahmeid,Kilwa Masoko   Familia moja ya Bw Bernad Towele dereva wa Gari la Takukuru Wilayani Kilwa Imenusurika baada ya Nyumba w...

KILWA MOTONa Abdulaziz Ahmeid,Kilwa Masoko 

Familia moja ya Bw Bernad Towele dereva wa Gari la Takukuru Wilayani Kilwa Imenusurika baada ya Nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia katika mji mdogo wa kilwa masoko.

Akithibitisha kutokea kwa tukio la Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 6 usiku kuamkia leo,Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,Joseph Mfungomara alieleza kuwa chanzo cha Moto huo bado hakijajulikana ila hakuna majeruhi.KILWA MOTO.2Kamanda Mfungomara alimalizia kuwa Vitu vyote vilivyomo katika nyumba hiyo vyenye thamani ya Tshs 7,700,000/ Havikuweza kuokolewa.

Baadhi ya Wananchi waliopo katika mji huo Akiwemo Mfanya biashara Ahmaid Shukra na Saidi Timamy mmiliki wa kituo cha Mafuta cha Alsat wameiomba Halmashauri hiyo kupeleka ombi maalum serikalini ili waletewe gari la Zimamoto kutokana na wilaya hiyo kuanza uwekezaji unaotokana na Raslimali ya Gesi ya Songosongo pamoja kukua kwa mji huo mashuhuri Afrika ya Mashariki

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top