Unknown Unknown Author
Title: MCHEZO WA YANGA Vs MBEYA CITY WAINGIZA TSH MIL 175, TFF KUSHEREHEKEA MIAKA 50 FIFA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TFF YAADHIMISHA MIAKA 50 FIFA Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaadhimisha miaka 50 tangu lipate uanachama wa Shirikisho la Ki...

clip_image001TFF YAADHIMISHA MIAKA 50 FIFA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaadhimisha miaka 50 tangu lipate uanachama wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (TFF) kwa shughuli mbalimbili ikiwemo michezo na makongamano.

Kamati maalumu itaundwa kwa ajili ya kupanga na kuratibu shughuli hiyo ambayo TFF imepanga kuadhimisha nchini nzima kwa kutumia wanachama wake.

TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) ilijiunga na FIFA Oktoba 8, 1964.

PAMBANO LA YANGA, MBEYA CITY LAINGIZA MIL 175

Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Yanga na Mbeya City lililofanyika jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 175,285,000.

Watazamaji 30,411 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Yanga ndiyo iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mgawanyo wa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 26,738,389.83, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,919,200 wakati kila klabu ilipata sh. 42,960,086.50.

Uwanja sh. 21,844,111.53, gharama za mechi sh. 13,106,466.92, Bodi ya Ligi sh. 13,106,466.92, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,553,233.46 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,096,959.36.

Nayo mechi ya Simba na Oljoro JKT iliyochezwa Februari 1 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 47,705,000 ambapo kila timu imepata sh. 11,254,122 kutokana na watazamaji 8,267.

Mgawanyo mwingine katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 4-0 ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 7,277,033.90 na gharama za kuchapa tiketi sh. 2,278,400.

Uwanja sh. 5,722,434.92, gharama za mechi sh. 3,433,460.95, Bodi ya Ligi sh. 3,433,460.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,716,730.47 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,335,234.81.

TFF YAPATA HATI YA KIWANJA TANGA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepata hati ya kiwanja chake kilichopo eneo la Mnyanjani katika Jiji la Tanga.

Hati hiyo ya miaka 99 ya kiwanja hicho namba 75 Block D chenye ukubwa wa ekari 7.6 ilikabidhiwa kwa TFF, Januari 13 mwaka huu.

Kiwanja hicho kitaendelezwa kwa matumizi mbalimbali, kubwa ikiwa ni uwanja wa mpira wa miguu.

Boniface Wambura Mgoyo

Ofisa Habari na MawasilianoShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top