Unknown Unknown Author
Title: HII NDIO RISALA KWA WASANII WA BONGO MOVIE WALIOJIUNGA NA CCM HAPO JANA, SOMA HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wengine sina shida nao... Ni haki yao kuchagua wanapopenda kwa interest zao na future yao. Ambacho kimenishangaza ni uamuzi wa Mjomba Mpoto...

clip_image001Wengine sina shida nao... Ni haki yao kuchagua wanapopenda kwa interest zao na future yao.

Ambacho kimenishangaza ni uamuzi wa Mjomba Mpoto... Nadhani ingefaa sana kama angekuwa neutral ili kulinda heshima ili raia kuona connection sanaa anayoifanya na dhamira halisi ya moyo wake..

Wako watu wengi wametunza siri za uanachama wao kwa vyama vyao ili kuendelea kunufaika na makundi yote katika jamii.

Politics is a game of opportunity, labda ameona fursa mahali.. Najua Sugu ameinspire wengi na ofcourse Chadema wamenufaika sana nae japo ni mmoja tu, Afande Sele anafanya vizuri pia akiishi alivyokuwa anahubiri.. Prof J pia nk. Natumai na hawa waigizaji wamefanya hesabu zao vizuri...

Hawatakuwa na wa kumlaumu kwasababu mchezo wa siasa unaweza kukukuza ama ukakuporomosha image yako..

Tukio limenikumbusha namna Nakaaya na Marlaw walivyokosea hesabu....

Nadhani misingi, nidhamu na heshima ya siasa zetu imeshusha hadhi na dhamana ya uongozi wa kisiasa. Kila mtu sasa akiwa maarufu tu utasikia anataka kuwa mbunge mahali fulani, hii ni bila kujali chama gani...

Ubunge umekuwa dili kutafuta utajiri wa haraka badala ya dhamana ya kuwakilisha raia. Urais ndio umefanywa rahisi kila mtu anahisi anaweza kuwa rais.

CREDIT:: BONGOCLANTZ

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top