Unknown Unknown Author
Title: MARLAW AKIPIGA CHINI CHAMA CHA CCM, ASEMA HANA MPANGO TENA….SOMA HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Marlaw Ajuta, Asema Hana Mpango wa Kushiriki Tena Kampeni za Kisiasa Dar es Salaam, Tanzania. Msanii wa kizazi kipya, Marlaw amesema kwamba...

Marlaw Ajuta, Asema Hana Mpango wa Kushiriki Tena Kampeni za Kisiasaclip_image001Dar es Salaam, Tanzania. Msanii wa kizazi kipya, Marlaw amesema kwamba kuanzia sasa hatajihusisha tena na shughuli za kisiasa kwani zimechangia kuporomosha muziki wake.

"Unajua mimi mwaka 2010 nimeburudisha katika kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini nimeambulia kushuka kimuziki sijui ni siasa imehusika au la kwa sababu tangu hapo nimetoa nyimbo nyingi, lakini hazivumi tena, sasa sitaipigia CCM tena labda chama kingine si unajua vijana wako wapi mzee ha ha haaa si kwamba nimejitoa ccm hapana mimi ni msanii naburudisha watu wote," amesema.

Msanii amehojiwa na gazeti la Mwananchi kuweka wazi msimamo wake, lakini alipoulizwa ni chama ganin amekikusudia kukipigia kampeni, alisema bado muda wa kutangaza, haujafika.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top