Unknown Unknown Author
Title: FRANK RIBERY,KARIMU BENZEMA WASHINDA KESI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MASTAA wawili wa kimataifa wa Ufaransa, Franck Ribery anayekipiga Bayern Munich ya Ujerumani na Karim Benzema wa Real Madrid ya Hispania, wa...

MASTAA wawili wa kimataifa wa Ufaransa, Franck Ribery anayekipiga Bayern Munich ya Ujerumani na Karim Benzema wa Real Madrid ya Hispania, wameachwa huru baada ya tuhuma za kufanya ngono na changudoa wa umri mdogo kutupwa Alhamisi.clip_image001Ribery, 30, alikiri kumlipa malaya huyo, Zahia Dehar kwa ajili ya kufanya naye ngono mwaka 2009, lakini akadai kuwa hakujua kuwa alikuwa na umri wa chini ya miaka 18 wakati huo.

Wakati Ribery akikiri kufanya ngono na Zahia, Benzema, 26, alikataa tuhuma zote, na mahakama ya jinai ya Paris ikaamuru kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha juu ya tukio hilo.

Umri wa ridhaa ya kufanya mapenzi nchini Ufaransa ni miaka 15, lakini kulipa fedha kwa ajili ya kufanya ngono na mtu wa chini ya miaka 18, kunatafsiriwa kuwa ni kufanya ngono na mtoto mdogo jambo ambalo ni kosa kisheria.

Ribery ambaye ana ndoa, Benzema na Zahia wote hawakuwapo mahakamani wakati hukumu ikitolewa.

HII SHERIA INGEKUWEPO TZ WANASOKA WETU WENGI WASINGEPONA!

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top