MAKAVU LIVE:: AKINA DADA WANAOJIONA WAZURI HII INAWAHUSU

Ukijaliwa kuwa Msichana mzuri na mrembo,usidhani utatetemesha kila Mwanaume, kuna wanaume na akili zao kichwani,urembo wako hauwasumbui, kama bichwa lako ni kanyaboya, uzuri wako hausaidii kitu, na utashangaa no one is paying attention, watu utakaowapata ni walewale kanyaboya wenzako, na hawana futuretabaki unaliwa bure kila siku unatoa macho.clip_image001Ukipata mwanaume anakupenda unaanza drama zako na kupiga watu danadana, madai yako hujali na unadhani hata akiondoka utapata mwingine kisa wewe ni mzuri, la hasha! Mwanaume akijitoa mhanga kukupenda kwa uzuri wako mheshimu, maana viumbe wa kike wakiwa wazuri ni shida na matatizo hakuna mtu anataka, sasa ukimwongezea na drama pamoja na yeye kujigeuza mpalestina kwako utajikuta umeolewa na kioo cha chumbani kwako, maana hicho ndo kinakudanganya sana kwamba we ni mrembo,

Watch out, drama zina mwisho,leo unacheza na mioyo ya watu unajiona we kifaa, usidhani wanaume hawaumii, tunaumia sema hatusemi tu, machozi yetu kama ya samaki, tunalia ndani kwa ndani

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post