Kwa mara nyingi tumekuwa tukiweka mambo mbali mbali ambayo yanaendelea katika jamii yetu ya Zanzibar,na mara nyingi tunapolalamika kuhusu uzembe wa serikali pamoja na ubadhirifu wa mali ya umma baadhi ya watu wanatwambia serikali si ya kulaumiwa, hivi majuzi tuliweza kwenda mental kwenda kumuangalia mmoja ya ndugu zetu ambae kalazwa huko na tukabahatika kupiga picha, hali inasikitisha jionee mwenyewe.Serikali imeona ni jambo la busara kwenda kujenga mnara wa Mapinduzi na kusaidia mabati, karata na mabao katika maskani za vyama vya siasa, wakati vijana walioathirika akili hawana hata magodoro ya kulalia, mlo wanayoipata ni miwili tu, asubuhi boflo kwa chai kavu na halikadhalika usiku pia ni boflo kwa chai kavu, hii ndio hali halisi.Wakati wanene wanaendesha magari makubwa makubwa ya pesa walizoiba kwa wananchi, na kujijengea majumba yenye thamani ya mamilioni ya shilingi, bila ya kujali umuhimu wa kuboresha vituo vya afya pamoja na elimu.Sote tukubali makosa kuwa jamii yetu imefeli kwa sababu wazembe tunaowachagua kutoka vyama vyote viwili hawana uchungu wala uzalendo wa nchi yetu, wote midomo mirefu kwa kusema lakini vitendo hakuna na tutabaki kuwa hivi hivi.Baada ya kufuatilia tuliambiwa kuwa serikali inatakiwa itoe milioni mbili kila mwezi kwa chakula katika spitali hii iliyopo kidongo chekundu lakini hakuna kinachofika zote zinaishia kwenye matumbo ya walio wachache.Ndugu mwananchi ukinafasika tembelea hospitali ya Kidongo Chekundu ukajionee hali ilivyo tunakuonya kama moyo wako laini tafadhali usiende.
SOURCE: VOICEOFZANZIBAR
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.