Unknown Unknown Author
Title: GONJWA LA AJABU LA WAKUMBA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI, WAANGUKA OVYO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
WANAFUNZI (15) wakiwemo wavulana na waschana wanaosoma Shule ya msingi Mtanda, katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, wamelazwa kituo cha ...

zahanatiWANAFUNZI (15) wakiwemo wavulana na waschana wanaosoma Shule ya msingi Mtanda, katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, wamelazwa kituo cha Afya cha mji huo, wakikabiliwa na tatizo la kuanguka na kupiga kelele ovyo.

Wanafunzi walikumbwa na ugonjwa huo, kuanzia darasa la tano, sita na saba, kuanzia darasa la nne hadi la saba, wamekumbwa na shida
hiyo, kuanzia saa 2:30 asubuhi, walipo kuwa madarasani wakiendelea na masomo.

Mwalimu mkuu wa Shule hiyo ya Mtanda,Twalibu Fadhili, ameliambia
gazeti hili eneo la kituo hicho cha Afya kuwa, wanafunzi waliokumbwa na tatizo hilo wapo waschana (12) na wavulana wawili.

Amesema wanafunzi hao waliokimbizwa kituo cha Afya mji Lindi na
madarasa yao kwenye mabano (7) ni wa darasa la tano,(4) la sita na (2) la darasa la saba.

Fadhili amesema tatizo la wanafunzi kuanguka kwenye Shule hiyo ya
Mtanda, ilianza rasmi mwezi Novemba mwaka 2013, kwa idadi ndogo ya watoto waliokuwa wakianguka kisha kupiga kele, ikiwemo maeneo ya mstarini au madarasani wanapokuwa wanasoma yao.
mtanda shule"Tatizo la aina hii limeanza kwenye Shule yenu Novemba mwaka jana, lakini sio kwa idadi kubwa ya watoto wanaoanguka, kwani walikuwa wanatokea wawili au watatu"Alisema Mwalimu fadhili.

Amesema wakati tatizo hilo linatokea, uongozi wa Shule uchukuwa jukumu la kuwajulisha wazazi au walezi wao ambao uwenda Shuleni na kuwachukuwa vijana wao, au uwarejesha makwao na kuwakabidhi wazazi wao kwa kuendelea na taratibu zingine, baadae watoto urejea Shuleni kuendelea na masomo yao.

Mwalimu huyo amesema kwa mwaka huu, hiyo ni mara ya pili kutokea tangu wafungue Shule hiyo wiki mbili zilizopita, ambapo uongozi wa Shule ukaamua kuwaita wazazi na wadau wa elimu ili kutafakari na kuchukuwa hatua ya kuweza kudhibiti hali hiyo isiendelee kutokea tena.

"Wakati najiandaa kuwaita wazazi tukutane na kulijadili suala hili, Leo tena limeendelea kutokea tena kwa idadi kubwa ya watoto, kwa kusema kweli inasikitisha sana"Alisema Mwalimu mkuu Fadhili.

Naye, mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Mtanda, Selevesta Simon, ambaye alikuwa katika watu walioongoza na msafara wa kusindikiza watoto hao, alisema wakati watoto hao wakiwa kwenye gari, baadhi yao walisikika wakisema "Huyo anatufuata na wengine wakitamka kuwa ndani ya darasa la nne kuna pembe na ndani yake mna damu".mtanda shule.2Mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha Afya cha mji, Dr. Enock
Chilumba, amekiri kupokea wanafunzi hao, na kueleza tatizo hilo
linatokana na Saikoroji ambayo mara nyingi uwakumba watoto
wanaokaribia kuwa na umri furani kuelekea kwenye utu uzima.

"Hiyo ni condition ambayo uwapata watoto wale watoto wanaoanza kubarehe, na hatimaye kuinvovu kwa watoto wengine hususani wale wanaokuwepo mahali pamoja"Alisema Dr.Chilumba.

Amewataja wanafunzi waliolazwa kuwa ni, Sharifa Mshamu, Zulfa Issa, Neema Silvester, Six Mrope, Fatu Jumanne, Magrethy Anthony, Anita Ngongi, Hadija Hassani, Vailet Mwaisaka, Brayani Kachenje.

Dr.Chilumba aliwataja wengine kwa jina moja moja kutokana na kushindwa kuongea kuwa ni, Zainabu, Suma, Rehema na hadija.

Mganga mfawidhi huyo wa kituo cha Afya amesema hii ni mara ya pili kwa kituo hicho kupokea wanafunzi wanaopatwa na matatizo ya aina
hiyo, kwani mwaka jana wanafunzi zaidi ya wanane wa Sekondari ya Ngongo nao walikumbwa na tatizo hilo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top