DIAMOND ALALAMIKA KUHUSU SHUTMA MBAYA DHIDI YAKE, SOMA ALICHOKISEMA LEO HII

clip_image002Hii ni dhahiri kwa msanii wa Bongo fleva Nasib Abdul amechoshwa na Maneno ya uzushi ya watu au wasanii wenzake dhidi yake, hii imethibitika kupitia akaunti ya msanii huyo ya Instagram kuamua kupost post ya Masikitiko kuhusiana na shutuma mbalimbali dhidi yake na amefunguka kama ifuatavyo:

"kiukweli, nasikitishwa sana jins baadhi ya wasanii kutwa wanavyolazimisha kunitengenezea ugomvi wa
kilazima pasipo kuwa na sababu, mara wengine wakizusha eti Nimewatusi kwenye Media, Mara sjui Nimepost kuwakashif, yaani ilimradi tu....kwanini Wanamuziki wa Tanzania Tunashindwa kubadilika...

Mbona mi nahangaika na muziki wangu kimpango wangu... Mnasema nyie ndio mnaojua kuimba mie sijui "sinatatizo"... Mnasema nyie ndio wenye sauti nzuri yangu mbaya "Sina tatizo"...

Sasa mbona tena bado mnanifatilia na kutokujua kwangu... Nafkiri ni vyema mkaanza kutumia ujuzi wenu kukuza sanaa ya nchi yetu na kuleta heshima na maendeleo nchini, kuliko kupika majungu..... Watu wanataka kazi!" Alimaliza kwa kusema hivyo Diamond Platnumz.DIAMOND STS

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post