Handsome Boy asiye na matunzo, Young Killer amesema video ya wimbo wake ‘Mrs Supastaa’ iliyoongozwa na Adam Juma ni moto wa kuotea mbali.
Rapper huyo kutoka Rock City amesema kuwa ikitoka mashabiki wake watasuuzika roho.
“Ni video kali, naamini katika video zangu zote ile ndio inaweza kuwa video yangu ya kwanza kufanya video kali. Naamini zingine zitakuja ila ile kiukweli kali yaani,” amesema Killer. “Nategemea mashabiki wangu wataipokea vizuri kwasababu ni video nzuri, binafsi nimeridhika nayo, sijawahi kufanya video kama ile.”
Tags
HABARI ZA WASANII