Unknown Unknown Author
Title: UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI CHAMA CHA CCM, NAMIKANGO - NACHINGWEA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Abdulaziz Video,Nachingwea, Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Lindi ambaye hivi karibuni alijiondoa kwenye chama hicho, Alli Chitan...

clip_image001Na Abdulaziz Video,Nachingwea,
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Lindi ambaye hivi karibuni alijiondoa kwenye chama hicho, Alli Chitanda ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi huku akiungwa na mkono na Katibu wa CUF wa Kata ya Namikango, Simoni Thomas Cosmas na wanachama wengine watatu wa CHADEMA walikabidhi kadi za vyama vyao na kutangaza kujiunga CCM.

Chitanda ambaye licha ya kushika nyazifa mbalimbali za juu kwenye
chama cha CHADEMA alitoa tamko hilo jana kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za udiwani wa kata ya Namikango wilaya ya Nachingwea, ambapo licha ya kuamua kuamia CCM pia alihadi kukifanyia kampeni Chama hicho kwenye mikutano yake yote itakayoifanya wakati wa kampeni iliyoizindua hadi itakapohakikisha kiti hicho cha Udiwani kata ya Namikango kinarejea tena CCM.

“Nimekuwa kwenye vyama vya upinzani kwa miaka mingi lakini tatizo la CHADEMA kinaendeshwa kama Kampuni ya mtu binafsi inayojali maslahi ya viongozi wachache binasfi huvyo ndugu zangu wananchi naomba kwa sana msikiunge mkono chama ambacho hakifuati maslahi ya watu hasa maskini”alisema Chitanda.

Akizungumza wakati baada ya kutambulishwa na Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe ambaye alikuwepo kwenye mkutano huo wa kampeni, Chitanda aliwataka vijana wanaokimbilia CHADEMA Kuanza kujihoji sana juu ya uamuzi huo kwani kimepoteza mwelekeo kutokana na viongozi wachache kukifanya chama hicho kuwa ni taasisi binafsi na kuwa licha ya kukitumikia chama hicho kwa zaidi ya miaka kumi ameamua kujiondoa.

“Kati ya watu ambao wamekaa muda mrefu na kushika nyazifa mbalimbali kwenye Vyama mbalimbali vya upinzani kuanzia NCCR hadi CHADEMA nimeamua kuachana na Vyama hivyo baada ya kubaini kuwa ni mali ya wachache kwa maslahi yao”alisema Chitanda,

Kauli ambayo iliungwa mkono na Akwilolmbe ambaye kabla ya kurejea Chama cha Mapinduzi aliwahi kuwa Naibu Katibu mkuu wa CUF na baadae kuwa pia Naibu katibu mkuu wa CHADEMA na kuamua kuachana na vyama hivyo kwa kile alichosema
kuchoshwa na vitendo vya ubinafsi, uchoyo wa madaraka unaofanywa na viongozi wa juu wa Vyama hivyo.

Akizindua Kampeni hizo kwenye mkutano uliuofanyika katika kijiji cha
Nangunde, Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Lindi, Mohamedi Mtopa aliwaomba wananchi wa Kata hiyo kumchagua mgombea wa chama hicho, Elias Mhagama ili aendeleze yale yote yaliyoanzishwa na Diwani wa awali ambaye amefariki dunia, Abdalah Mbinga na kuwa uchaguzi huo ni wa kujaza nafasi hivyo umakini katika kutoa maamuzi unatakiwa badala ya kufanya chaguzi kwa ushabiki.

“Chagueni mtu makini na si kwa ushabiki kwani uchaguzi ni maisha si mchezo wa mpira kuamua kwa kushabikia itawagharimu naomba muwe makini na umakini huo utaonekana pale mtakapo mchagua mgombea wa Chama cha Mapinduzi”alisema Mtopa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top