TAARIFA KAMILI KUHUSU AJALI ILIYOUWA WANAFUNZI 5 WA SABODO MKOANI MTWARA

clip_image001Wanafunzi watano wa shule ya sekondari Mustafa Sabodo iliyopo nje kidogo ya mji wa Mtwara wamefariki Dunia na wengine 47 kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari wakati  wakikimbia mchakamchaka mapema leo asubuhi.clip_image001[8]Taarifa inasema kuwa gari hilo lenye namba za usajili T174 AED aina ya Mercides Benz lilikuwa likiendeshwa na dereva Baraka Mgwegwe ambapo likiwa kwenye mwendo kasi liliacha njia na kuwagonga wanafunzi hao ambao walikuwa kandokando ya barabara wakikimbia mchakamchaka kurejea shuleni.clip_image001[10]Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Zelothe Steven na Mganga Mkuu wa hospital hiyo wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amewataja wanafunzi waliopoteza maisha kwa ajali hiyo ni pamoja na Khairati Mohamed Said, Mwanahamisi Mohamed, Nasma Salum Mpunja, Hilda Matias Nguli na Farida Ally ambao wote wanasoma kidato cha kwanza katika shule hiyo.clip_image001[6]Mpaka sasa hali za majeruhi 21  waliolazwa hospitalini hapo zinaendelea vizuri ukiondoa mmoja ambaye amehamishiwa katika hospitali ya mission Nyangao mkoani Lindi kwa matibabu Zaidi huku dereva aliyesababisha ajali hiyo akishikiliwa na polisi kusubiri sheria kufuata mkondo wake.clip_image001[12]
Haya ni Majina ya Majeruhi::
EVA MADEBE, ASHURA ZUBERI, ALLY YUSUF, HAMZA HAMIS, MARGRETH MAIKO, TUMAINI DADI, LATIFA EMMY, SELEMAN NAMBOA, BAKARI LEBA, FARIDA HAMIS, MWANAIDI SAIDI, MAY KENETH, SHAMIRA SAIDI, NASMA HAMIS, EVA ISSAYA, JAZIRA SAIDI, GAUDENCE LEONARD, RAMADHAN PARIS, BAKARI
NASORO, ALEH MPELEMBE, FATUMA ISMAIL, KARIMA KILEMA, HILDA SETA. SHARIFA AHMAID, BAKARI MATHEW, MUSA NGATEULA, ROSE GODWIN, RAHMA HASHIM, FATUMA AZIZ, CHRISTOPHER BOSCO, HAMZA HAMIS, TUMAIN LABAN, FATUMA ALLY, YOWERI SAIMON, RAMADHAN MTIPA, NEEMA MOHAMED


CREDIT TO Millardayo.com

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post