SHAA AFUNGUKA KUHUSU KOLABO ZA KIMATAIFA, SOMA HAPA ALICHOSEMA

Sarah Kaisi aka Shaa anahisi kolabo nyingi za kimataifa ni za kulazimisha, hugharimu fedha nyingi na wala hazina manufaa kwa wasanii wengi wa Kibongo.clip_image001Akiongea na safu ya Starehe ya gazeti la Mwanancho, Shaa amesema hana mpango wa kufanya kolabo za aina hiyo.

“Siwezi kufanya kolabo na staa yeyote wa kimataifa,” alisema.

Mimi nipo kibiashara zaidi na ni ngumu kwangu kwa sababu nahitaji kufanya muziki nipate fedha. Hizi kolabo za kimataifa unajikuta ukimlipa pesa mhusika huku wewe ukiingia gharama ya kusafiri huko na kurekodi.

Kama unavyojua, inachukua muda na gharama kubwa, nahitaji kufanya kitu ambacho nitafaidika nacho na siyo kunipotezea fedha.”

“Asilimia kubwa kolabo hizo ni za kulazimisha na kupoteza pesa, siyo za kuuza au kumwingizia kipato mhusika. Unatakiwa ufanye kolabo, kisha upate shoo kubwa za kurudisha gharama uliyotumia. Lakini nionavyo mimi nyingi ni za kutafuta ujiko tu, siwezi kufanya kolabo na D Banj kisha isiniingizie chochote.”

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post