HATIMAYE BABY MADAHA AKIRI KUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA BOSI WA CANDY n CANDY

clip_image001Baby Madaha na Joe Kairuki

Utakubaliana nasi kuwa huduma na mashavu anayoyapata Baby Madaha kutoka kwa bosi wa Candy n Candy Records, Joe Kariuki ni zaidi ya msanii aliyechukuliwa kuwa chini ya label hiyo kiasi ambacho kimewafanya wasanii wengine wa label hiyo wanune kwa jinsi msanii huyo wa Tanzania anavyopendelewa.

Uhusiano wa Baby na Joe ni unaenda zaidi ya msanii na meneja wake. Wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi.

“Uhusiano wangu na Joe mmmh…Joe amekua zaidi ya meneja wangu,” Baby aliliambia jarida la Spice la nchini Kenya.

Natumia muda mwingi nikiwa naye. Kwanza kabisa, sijali kile watu wanasema. Mi namuona anavutia na mchangamfu. Pili nina furaha. Na kama uhusiano wangu na Joe hauniathiri kwanini nimsumbue mwingine? Mwisho, kama yupo single, kipi kibaya sisi kuwa na uhusiano?”

Source: BONGO 5

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post