Baadhi ya madiwani waliokutana na waandishi wa Habari kutoa
tamko la kumtaka Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Lindi kuitisha kikao
maalum ndani ya siku 14 ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya madai ya
madiwani
Na. Abdullaziz Video, Lindi
Madiwani 14 kati ya 25 wa Manispaa ya Lindi wamejiorodhesha na
kuandika barua kwa Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo kumtaka kuitisha kikao maalum cha Baraza la madiwani ili kupata taarifa mbalimbali ikiwemo hatua ya Mkuu wa Mkoa kufunga Ofisi ya Mipango Miji kwa zaidi ya mwezi mmoja pamoja na kuanza kwa mauzo ya Viwanja huku madiwani wakiwa hawana taarifa.
Akiongea na waandishi wa Habari, Diwani wa kata ya Nachingwea, Omary Chitanda alieleza kushangazwa na hatua ya mkuu wa mkoa kufunga ofisi ya Idara ya Mipango Miji kwa zaidi ya mwezi mmoja kinyume na taratibu za ofisi za serikali
“Sisi ndio Halmashauri ila imetushangaza sana Kitendo cha mkuu wa mkoa kufunga ofisi ya mipango miji na kuunda tume ambayo ilimaliza kazi ila sisi madiwani tumeomba taarifa ya Tume hiyo atupewi akaunda tume tena kuhusiana na mgogoro wa wananchi na manispaa kuhusiana na ardhi iliyochukuliwa katika mpango wa UTT Pia madiwani atupewi taarifa. Je sisi kweli ni wawakilishi wa wananchi tunafichwa hivi? alielezaChitanda
Pamoja na hilo Madiwani hao walieleza kusikitishwa na kutofahamishwa na hatma ya Vibanda 8 vilivyojengwa katika eneo la kituo cha mabasi na baadhi ya madiwani kinyume na utaratibu na kuzuiwa na manispaa hiyo kwa muda mrefu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi
Jitihada za kumpata mkuu wa mkoa Lindi, Ludovick Mwananzila ana kwa ana hazikuzaa matunda na kufanikiwa kumpata kwa njia ya Simu ambapo alikiri na kueleza kuwa tayari ameshatoa maelekezo kwa Meya na Mkurugenzi wa manispaa kwa utekelezaji na pia Taarifa ya Tume zake amewasilisha Tamisemi na kwa Waziri Mkuu.
Hivi karibuni Ofisi ya Manispaa ya Lindi imeanza kutangaza kupitia
vyombo vya habari kuhusiana na Uuzaji wa Viwanja katika maeneo ya
mmongo, Mabano na Mitwero chini ya mpango uliofadhiliwa na UTT
Madiwani waliojiorodhesha na barua yao Ni kama inavyosomeka na sahihi zaoBarua ya Madiwani kwenda kwa mstahiki Meya