Unknown Unknown Author
Title: LIGI DARAJA LA TATU NGAZI YA MKOA:: KUSINI SOCCER MOTO WA KUOTEA MBALI YAINYUKA KILWA STARS 4 - 0
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ligi Daraja la Tatu Ngazi ya Mkoa Mkoani Lindi inafikia Patamu Baada ya Leo hii Timu ya Kusini Soccer Kujikusanyia Point 6 na kuwa kinara w...

Ligi Daraja la Tatu Ngazi ya Mkoa Mkoani Lindi inafikia Patamu Baada ya Leo hii Timu ya Kusini Soccer Kujikusanyia Point 6 na kuwa kinara wa ligi hiyo kwa jumla ya magori Manane huku Kariakoo FC ikiondolewa katika Nafasi ya kwanza ya ligi hiyo kwa kuwa na Point 6 na Magoli 4 na kushika nafasi ya pili.

DSC07081Kikosi Cha timu ya Kusini Soccer kilichocheza hii leo dhidi ya Kilwa Stars

Kusini Soccer iliingia uwanjani leo hii kuivaa timu ya Kilwa Stars iliyona makazi wilaya ya Kilwa huku bechi la Ufundi likiwa na mapungufu ya kutokuwepo kwa kocha Mkuu wa timu hiyo sababu zikielezwa kuwa Kocha huyo alitiliwa Mashaka kwa kupanga kikosi zaifu kabla ya mechi hiyo hivyo wachezaji wakalalamikia uamuzi huo na kusikilizwa na Uongozi wa timu hiyo na kuamuliwa kuwekwa pembeni katika mchezo huo.

Kocha huyo alionekana Katika Jukwaa la washangiliaji na kuwashangaza wengi waliohudhuria mchezo huo bila ya kuwa na Majibu hadi pale mtu wa karibu na uongozi huo alipotoboa siri hiyo kwa sharti la kutotajwa Jina.

DSC07082Bechi la Ufundi la timu ya Kusini Soccer katika mechi dhidi ya Kilwa Stars

Mpira ulianza kwa kwasi huku Vijana wa Kilwa Stars Kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini waliwezwa kupunguzwa kuvu na beki maridadi ya Timu ya Kusini Soccer kwani ilikuwa makini kuondoa Hatari iliyojitokeza langoni mwao

Iliwachukua dakika 13 tu Timu ya Kusini Soccer kupata goli la kwanza kupitia Mchezaji wao machachari anaevaa jezi namba 5 Muksini Abdallah ambaye alimchamvua golikipa mahiri wa timu ya Kilwa Stars na kuandika goli hilo la Kuongoza.

DSC07084Benchi la Ufundi Timu ya Kilwa Stars katika Mechi dhidi ya Kusini Soccer

Baada ya Dakika 5 mshambuliaji Msafiri Kambwili aliwezakuwapatia raha mashabiki wa Timu hiyo ya Kusini Soccer Goli la Pili baada ya kupokea pasi saafi na bila pupa akaweka mpira kwenye nyavu kwani tayari Golikipa alikuwa amesha toka golini na kufanya Matokeo hayo hadi dakika ya 18 ya Mchezo kusomeka 2 – 0. matokeo hayo yalidumu hadi kipindi cha mapumziko.

DSC07085Kocha wa Kilwa Stars akiwapa maelekezo Vijana wake wakati wa Mechi kati ya Kusini Soccer na Kilwa Stars ambapo Kusini Soccer walishinda 4 - 0

Kipindi cha Pili kilianza kwa Kusini Soccer Kuonyesha Kandanda la Kurizika kwani hawakutumia nguvu tena kusaka mipira wala kushambulia kwani walijiona tayari wamemaliza mchezo huo kwa kuzingati timu pinzani haikuonyesha makali yeyote langoni mwao hivyo kufanya mpira huo kupooza na mipira mingi kupotea. Hali hiyo iliwafanya Kilwa Stars Kupata nafasi ya kushambulia hasa baada ya Mchezaji mahiri wa Kusini Soccer kuumia na kutolewa nje na kufanyiwa mabadiliko sehemu ya kiungo lakini hawakuweza kupata Goli.

DSC07089Mashabiki walifurika uwanja wa ILULU kushihdiaa mtanange huu baina ya Kusini Soccer 4 – 0 Kilwa StarsDSC07090

Ni frank Ngomo aliiandikia Bao la 3 Timu ya Kusini Soccer mnamo dakika ya 53 ya mchezo baada ya timu hiyo kupiga one two katika eneo la hatari la timu ya Kilwa na kufanikiwa kuweka mpira huo nyavuni.

Dakika 2 ya nyongeza iliweza kuwa mbaya kwa timu ya Kilwa Stars Baada ya Mchezaji Abdallah Kipara kupata mpira mzuri katika eneo la Kumi na nane na kuachia shuti kali katika upande wa pembeni wa Lango (side net) la Kilwa Stars na Mpira huo kuingia ndani ya nyavu tukio hilo liliweza kumshawishi refa wa mchezo huo ndg: Peter Mlungusye kuweka mpira katikati kuashiria ni goli, DSC07083Lakini watu walio karibu na Goli hilo walikataa na kusema lilikuwa si goli kwani mpira huo uliiingia golini kupitia kwa nje ya goli sehemu hiyo nyavu ilikuwa imechanika, lakini Refa Hakubadili maamuzi yake na kuweka mpira katikati na kufanya matokeo hayo kuwa Goli 4 – 0.DSC07055Ligi Hiyo Itaendelea tena Tarehe 11/01/2014 kwa kuzikutanisha timu ambazo zimekuwa vibonde kwa timu za Kariakoo na Kusini ambazo ni Kilwa Stars Vs Captown.

Bila kusahau Siku ya Jumapili itakuwa Vuta nikuvute katika uwanja wa Ilulu kwani itakuwa ni Derby moja kali kutokana na Timu hizo kuwana upinzani wa hali ya juu ambapo zitakutana timu za Kariakoo Fc Vs Kusini Soccer

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top