Katika Michezo ya awali Kariakoo Fc iliweza kuifunga Kilwa Stars Mabao 3 – 0 na kujikusanyia point tatu na kuwa timu ya pili katika Msimamo wa ligi hiyo kabla ya mechi ya leo hii.
CapTown nao wako katika hali mbaya kwa kukubali kufungwa mechi ya kwanza na timu ya Kusini Soccer ambayo ndio kinara wa Ligi hiyo kwa kuwa na Magoli mengi kwani walijikusanyia magoli hayo kwa kuifunga CapTown magoli 4 – 0 katika mechi yao ya Fungua Dimba.
Ili iweze kusonga Mbele Timu ya CapTown inabidi washinde michezo iliyobaki na huku wakiombea Timu za Kusini Soccer kupoteza mchezo wake dhidi ya Kilwa Stars na dhidi ya Kariakoo Fc.
Mchezo wa Kesho unatarajia kuwa Mgumu pia kwani Kilwa Stars wanaingia Uwanjani huku wakiwa hawana Point wala goli hata moja hivyo kutawafanya kutafuta Point Tatu muhimu kwa udi na uvumba ili kurejesha matumaini yaliyopotea ya kusonga mbele katika Michuano hiyo.
Kumbuka Mechi ya kesho itawajia LIVE kupitia Page yetu ya Facebook Hivyo Kama huja Like page yetu Huu ni muda muafaka ili usipitwe na UPDATES ZA RIPORTER WETU. Bofya Hapa
Tags
SPORTS NEWS