Mchezaji wa Manchester United Wilfried Zaha imeripotiwa kuwa anakamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Cardiff City kwa kipindichote cha msimu uliobakia.
Zaha, ambaye alijiunga na United akitokea Crystal Palace kwa uhamisho wa 15 million-pound mwaka jana, amefanyiwa vipimo vya afya na timu hiyo inayofundishwa na mshambuliaji wa zamani wa United Ole Gunnar Solskjaer.
Gazeti hilo limeandika kuwa mchezaji huyo ameonekana akiingia kwenye hospitali huko Cardiff kwa ajili ya kufanyiwa vipimo. anategemewa kwamba ataweza kuanza katika mchezo wake wa kwanza na Cardiff dhidi ya Norwich City mnamo Feb. 1.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.