Los Angeles, Marekani
Wakati kikwetu kwetu, mtu kuwa mnene wakati mwingine kunatafsiri kwamba una afya njema, au mambo yako yako sawa, mkali wa R&B kutoka USA, na mke wa rapa Jay Z, Beyonce Knoewles(Pichani), amefunguka kuhusu jinsi asivyoutaka unene, unene kwa kusema kuwa anapenda kuwa na shepu lakini siyo kunenepa.
Kimsingi alionesha wazi kwamba hapendi kuwa kimbaumbau, lakini hapendi kuwa mnene utakaosababisha kupotea kwa mpangilio wa viungo vyake, kiasi kwamba hadi asijulikane mwili wake ulipoanzia na kuishia.
“Tangu nikiwa msichana napambana na mwili, lakini ningejiachia mimi ni mnene sana, napambana kwa kuwa nataka kila kiungo kiwe na nafasi yake, nakuwa makini nisikonde sana nikawa kama mwanamitindo”alisema Beyonce alipokuwa kwenye mahojiano na mtandao wa E! Online.
Aliongeza kuwa licha ya kuwa mama wa mtoto mmoja, bado anahitaji kuwa na muonekano mzuri mbele ya mumewe Jay Z.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.