Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndg Ludovick Mwananzila na Mkurugenzi wa MEIS ndg Merey Ally Saleh wakati wa Uwekaji Jiwe la msingi la Kiwanda Cha Sementi Kiitwacho MEIS LINDI CEMENT Mkoani Lindi.Mh. Pinda Akiweka Sahihi katika Kitabu cha wageni wakati wa Ziara yake katika Kiwanda cha MEIS LINDI CEMENT katika uwekaji wa Jiwa la msingi la kiwanda hicho hivi leo.Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akipata Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa MEIS LINDI CEMENT jinsi hatua iliyofikiwa hadi sasa katika Kiwanda Hicho wakati alipotembelea kiwandani hapo Leo hii katika Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kiwanda Hicho.Hatua iliyopo kwa hivi sasa hakika Kiwanda kinapiga Hatua na kitaweza kumalizika kujengwa kwa wakati kwani Vifaa vyake vyote asilimia 90 tayari Vimewasili nchini na Vipo katika eneo la Kiwanda Hicho.Kiwanda hichi kinatarajia kuwapa wananchi zaidi ya 2000 ajira na kufanya kupunguza tatizo la Ajira hasa kwa wananchi wa Lindi na Mikoa ya Kusini kwa ujumla.. sasa tayari wafanyakazi 250 wamepatiwa ajira katika kipindi hiki cha Mradi wa Ujenzi.Huu ndio muonekano wa Kiwanda cha MEIS LINDI CEMENT utakavyo kuwa mara baada ya Ujenzi wake Kukamilika.Wananchi walio Hudhuria Hafla Hiyo ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Kiwanda Cha MEIS LINDI CEMENT hivi leo. ufunguzi huo umefanywa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akifuatana na Mama Pinda Pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Mh. Sospeter Muhongo
Home
»
HABARI ZA KITAIFA
» HABARI KATIKA PICHA: WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA SEMENTI MKOANI LINDI
About Author
JE, UNA HABARI, PICHA, TANGAZO, MAKALA NA USHAURI? USISITE KUWASILIANA NASI SIMU / WHATSAPP NAMBA 0625535420.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.