Musa Mateja na Khadija Mngwai
WAKATI kikosi cha Yanga kikitarajiwa kuwasili nchini leo alfajiri kutoka Uturuki kilipokuwa kimeweka kambi kwa muda wa wiki mbili, sakata la kiungo wa timu hiyo, Athumani Idd ‘Chuji’ limeonekana kutozingatiwa ambapo hakuna anayefuatilia juu ya adhabu yake.
Chuji alisimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu, hakwenda Uturuki ambapo wenzake walikuwa huko wakijiandaa na raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara inayoanza kesho Jumamosi na ushiriki wa michuano ya kimataifa.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu alipoulizwa na gazeti hili juu ya majaaliwa ya Chuji, alisema hana jibu wala ufafanuzi juu ya adhabu ya mkongwe huyo.
“Ligi si bado haijaanza, hivyo subiri ikianza utajulishwa, naombeni mvute subira hadi Januari 25 ambapo ligi itakuwa inaanza kisha mtajua,” alisema.
Njovu aliongeza kuwa, ratiba ya ndege inaonyesha kuwa msafara huo utawasili alfajiri leo, ambapo wakitua moja kwa moja wataingia kambini kujiandaa na mechi ya Jumamosi dhidi ya Ashanti United.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.