Unknown Unknown Author
Title: HABARI KAMILI: UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA MEIS LINDI CEMENT
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waziri Mkuu,Mhe Mizengo Pinda akifunua pazia kama ishara ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kiwanda cha MEIS Cement Lindi,wakati wa ziara...

PINDA AT MEIS LINDI 13Waziri Mkuu,Mhe Mizengo Pinda akifunua pazia kama ishara ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kiwanda cha MEIS Cement Lindi,wakati wa ziara yake ya siku mbili katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara .PINDA AT MEIS LINDI 14Waziri mkuu Mhe Mizengo Pinda akiwasili  kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha saruji Lindi na kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Merey ally SalehPINDA AT MEIS LINDI 15Waziri mkuu akizungumza na wakazi wa mji wa Lindi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha saruji Lindi na kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho,Merey ally Saleh

PINDA AT MEIS LINDI 16Timu ya mafundi ikongozwa na wachina katika hatua za ujenzi PINDA AT MEIS LINDI 18wadauPINDA AT MEIS LINDI 17Wananchi waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika eneo la Machole kinapojegwa kiwanda hichoPINDA AT MEIS LINDI 19Sehemu ya mitambo ya ujenzi.PINDA AT MEIS LINDI 6Mchoro wa kitakavyokuwa kiwanda hicho mara baada ya kukamilika mwishoni mwa mwaka huuPINDA AT MEIS LINDI 11Mandhari  ya kiwanda hicho katika hatua ya ujenzi inayotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu

Na Abdulaziz Video, Lindi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mizengo Pinda ameanza ziara ya siku mbili kukagua ujenzi wa bomba la gesi kwa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara ambapo pia aliweka jiwe la Msingi la ujenzi wa kiwanda cha Saruji cha Mjini Lindi.

Lengo la ziara hiyo ni kujionea maendeleo ya ujenzi wa bomba hilo ikiwa pamoja na kukagua ujenzi wa Viwanda 2 vya saruji cha Meis Lindi na Dangote cement cha Mkoani Mtwara.

Akiongea na wananchi na wafanyakazi wa kiwanda cha Meis Lindi,Waziri mkuu aliwataka wakazi wa mikoa hiyo kuchangamkia fursa hizo zilizopatikana ikiwemo kuongezeka kwa ajira Kwa wakazi wa Mikoa ya kusini kutokana na upatikanaji wa saruji hiyo.

Awali akimkaribisha waziri Mkuu kusalimia wananchi,Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila alimuomba waziri wa Nishati na Madini kupitia kwa waziri mkuu kuharakisha mpango wa matoleo ktk bomba la gesi ili gesi hiyo itumike kiwandani na majumbani ili kupunguza makali ya maisha kupitia nishati hiyo.

Kufuatia ombi hilo,Waziri wa Nishati na Madini,Sospeter Muhongo alibainisha kuhusiana na mpango huo ikiwemo Wizara yake kusaidia upatikanaji wa Umeme katika vijiji vilivyopitiwa na bomba hilo huku akiwaomba wana Lindi kuanza kujiunganisha kutumia umeme kutokana na punguzo lililopo.

Naye Meneja Mradi Wa Meis Cement,Valerian Magembe akisoma taarifa fupi ya ujenzi huo licha ya kuioomba serikali kuhusiana na upatikanaji wa haraka wa gesi hiyo pia aliwaakikishia wakazi wa Lindi kuwa kiwanda kitakamilika na kuanza kazi mwishoni mwa mwaka huu ambapo alibainisha kuwasili kwa asilimia 90 ya vifaa vya ujenzi Bomba hilo linalojengwa kutoka Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam lina urefu wa kilomita 542 na linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu Katika ziara hiyo.

Mh. Pinda ameambatana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa China nchini, Lu Youqing na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top