Msanii wa filamu nchini, Kulwa Kikumba maarufu kama Dude amesema mwaka 2013 aliufunga kwa matatizo baada ya filamu yake mpya kupotelea kwenye External ambayo alikuwa amehifadhi.Dude amesema amefunga mwaka kwa majonzi baada kifaa hicho kinachotumika kuhifadhia mafaili mbalimbali (soft copy) kuharibika na kushindwa kuokoa kitu.
“Kama unavyojua wasanii wa filamu, hasara ya milioni 7 ni pengo kubwa. Kwahiyo filamu ilimalizika salama, ilikuwa kwenye marekebisho ya mwisho ndipo likatokea tatizo la kuharibika kile kifaa ambacho nilihifadhia filamu. Niliishiwa nguvu yaani nimeumia sana na kuniharibia mipango yangu mipya ya mwaka mpya,” amesema Dude.
“Kufungua mwaka huu nilitaka kuanza na kurusha vipindi vyangu vya Bongo Dar es Salaam EATV, ila nimeshindwa kutokana na hasara niliyopata mwisho wa mwaka uliopita. Kwahiyo nategemea mipango ikikaa vizuri mwezi wa 3 Bongo Dar es salam itaendelea.”
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.