Unknown Unknown Author
Title: BOTI ILIYONUSURIKA KUZAMA YAWASILI ZANZIBAR SALAMA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kwa mujibu wa Abiria waliohojiwa wanasema Boti ya Kilimanjaro II ikitokea Pemba kuelekea Unguja imepigwa na dhoruba leo Jan 5 2014 kwenye sa...

clip_image001Kwa mujibu wa Abiria waliohojiwa wanasema Boti ya Kilimanjaro II ikitokea Pemba kuelekea Unguja imepigwa na dhoruba leo Jan 5 2014 kwenye saa nne asubuhi na kuponea kuzama ilipokua kwenye eneo hatari la Nungwi ambapo ilizama kidogo mbele na kunyanyuka hivyo watu wa mbele wote wakaachwa lakini pamoja na kuwatupa hao watu kwenye maji Nahodha akafanya uamuzi mwingine mgumu.

clip_image001Aliona akisimama ili kuwaokoa wale watu boti yote ingezama pale hivyo akaamua kuendelea na safari lakini kabla ya kuondoka watu kadhaa ndani ya boti wakajitolea kuwatupia life jacket wale waliotupwa kwenye maji ambapo shuhuda anasema kama mtu hajui kuogelea anaweza kupoteza maisha kwa sababu hawakua wamejiandaa kwenye tukio hili la ghafla na sio wote wamepata vifaa hivyo vya kujiokoa.

clip_image001[6]Shuhuda mmoja anasema ‘yani boti ilizama ghafla mbele hivyo watu wakatupwa kwenye maji kwenye hii sehemu ambayo kuna mkondo wa maji, upepo ulikua mkali sana yani unaona watu wanajaribu kujiokoa mabegi na vitu vingine vinaonekana juu ya maji’

Hali ilivyo ndani ya boti ambayo imeendelea na safari ni watu kujawa na huzuni na wengine wamebaki wanalia tu.

KAULI YA POLISI KUHUSU TAARIFA YA ABIRIA 10 WALIOTUPWA MAJINI

Kuhusu taarifa za watu 10 kurushwa baharini wakati upepo mkali ulipotokea, Polisi wanasema ‘hakuna mtu yeyote aliedondoka baharini na hizi taarifa ni kwa mujibu wa Captain wa boti hii N. Abubakar’

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top