BASI Likiwa limeanguka na maiti bado zilikuwa hazijatolewa chini
Baadhi ya abiria ambao walikuwemo katika basi hilo wakiwa wametoka bila kujeruhiwaBaadhi ya wananchi wakitoa msaada wa kubeba maiti kutoka
katika tukio kwa ajili ya kuzifikisha katika hosp ya Rufaa ya sokoine
LindiKamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi,Renatha
Mzinga akisimamia zoezi la kuinua basi hilo kwa ajili ya utoaji wa
Maiti 9 za ajali hiyo
Na Abdullazizi Video, Lindi
Watu 9 wakiwemo watoto 2 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30
kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la Alhamdulilah linalofanya
safari zake kutoka jijini Dar kwenda mkoani Mtwara kupinduka katika
kijiji cha Mambulu Manispaa ya Lindi.
Ajali hiyo iliyotokea mchana leo baada ya basi hilo kupishana na lori
na kupoteza mwelekeo na kupinduka hali ilichangiwa na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha
Hadi ninatoka eneo la tukio marehemu hao hawakuweza kufahamika kwa haraka kutokana na kukatika viungo na tayari majeruhi na maiti zote Waliofariki katika ajali hiyo zimefikishwa Hospitali ya Mkoa.
Naye kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi, George Mwakajinga ambae alikuwepo katika ajali hiyo hakuweza kuongea lolote kutokana na harakati za kuokoa majeruhi wa Ajali hiyo.
Taarifa zaidi za majeruhi hao pamoja na maiti zilizotambuliwa tutawajuza Baadae.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.