AGNES HOKORORO (MB) DC RUANGWA::AWATAKA WANANCHI WAKE KUJIUNGA NA CHF

clip_image001Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Fortunata Raymond  akiwaeleza wanahabari (hawapo pichani) namna ya utekelezaji wa zoezi la uhamasishaji wa wananchi kujiunga na CHF utakavyoendeshwa,sambamba na  mafanikio yanayotarajiwa kutokana na mkakati wa pamoja wa Mfuko na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa ulivyokusudiwa.Nawaambieni CHF ndiyo mkombozi wa huduma za matibabu sasa…Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Agnes Hokororo (MB) akitoa rai kwa wananchi wake Wilayani humo wakati wa uzinduzi wa kampeni za uhamasishaji wananchi kujiunga na CHF ulioenda sambamba na upimaji wa afya bure chini ya uratibu wa NHIF Lindi uliofanyika  leo hii kwenye viwanja vya CWT Ruangwa.Upimaji wa afya bure ukiendelea,madaktari wa mfuko na hospitali ya wilaya wameendelea kutoa huduma za uwiano wa uzito wa mwili (BMI),shinikizo la damu (BP) na sukari ambapo suala la lishe na shinikizo la damu (BP)ni changamoto iliyoweza kubainika hivyo ushauri ulitolewa,kushoto ni Dr. Rashida Omari wa hospitali ya wilaya akimpima kiwango cha sukari mzee Abdalah Ngawenje.

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Agnes Hokoro (MB) akipima BMI kwenye viwanja vya CWT,anayempima ni afisa wa mfuko ofisi ya mkoa wa Lindi Laurent Hoja.Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya Agness Hokoro hayupo pichani wakati wa uzinduzi huo .

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post