VICTORIA KIMANI AMSIFIA VANESA MDEE KATIKA SHOW YA “RHYTHM UNPLUGGED” HUKO NIGERIA

clip_image002Jukwaa la ‘Rhythm Unplugged’

Weekend iliyopita msanii wa Tanzania Vanessa Mdee a.k.a Vee Money alikuwa nchini Nigeria kwa ajili ya kuhudhuria na kutumbuiza katika show kubwa ya mara moja kwa mwaka, ambayo huwakutanisha wasanii wa A-list wa nchi hiyo katika jukwaa moja.

clip_image002[7]Baada ya show hiyo Vanessa alipost picha Instagram akiwa na dancers wa Naija waliopanda naye jukwaani kumpa support na kuandika;

“These ladies gave me LIFE tonight S/O to Nigeria’s CLIMAX dancers! What a stage, what an audience, what a show, what a slayin!!!! THANKYOU JESUS!!!!”.

clip_image002Victoria Kimani

Naye msanii wa Kenya mwenye makazi nchini Nigeria Victoria Kimani, kupitia Instagram aliandika kuwa kati ya vitu alivyovipenda kwenye tamasha hilo ni pamoja na show ya Vee Money ambaye ameiwakilisha vizuri Afrika Mashariki.

clip_image002[9]“My Favorite Part of the Show from Top Left: My Gals @ceodancers Killed it as usual! @2faceidibia1 THE YOUNG LEGEND … Wycleff Jean Shut it Down! And my girl @vanessamdee Made me Proud! She repped East Africa well #Nigeria #Tanzania #Haiti #SouthAfrica #Kenya #RhythmUnplugged” aliandika Victoria.

Rhythm Unplugged ni show iliyofanyika Jumapili iliyopita Lagos, Nigeria na kuwakutanisha wasanii wakubwa wa Naija katika jukwaa moja wakiwemo 2Face, P-Square, WizKid, D’Banj, Davido na wengine. Host wa show hiyo kwa mwaka huu alikuwa nyota wa kimataifa Wyclef Jean.

SOURCE: BONGO 5

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post