Ligi daraja la Tatu ngazi ya Mkoa wa Lindi imeendelea leo hii kwa kuzikutanisha timu pinzani hapa mjini lindi ambazo ni Kariakoo Fc na Kusini Soccer zote zikiwa na mashabiki lukuki.
Mchezo wa leo ulikuwa wa aina yake kwani ushindani ulikuwa mkubwa kwa timu zote mbili zikitafuta nafasi ya Kwanza ya kuongoza ligi hiyo, Kariakoo Fc ikiwa inshikilia uskani wa ligi hiyo kwa Point 11 Huku timu ya inayoshika nafasi ya pili ni Kusini Soccer yenye point 9. Hii ni baada ya Mchezo wa Leo kumalizika kwa Sare ya Bila kufungana.
Mchezo huo ulianza kwa Kasi kwa Pande zote kushambuliana kwa zamu lakini beki wa pande zote mbili walionyesha umakini kwa kuzuia hatari zilizojitokeza langoni mwao. Lakini Mechi hiyo ilijaa rafu za hapa na pale lakini mwamuzi Miaraji Mlaponi alionekana mpole kwa kushindwa kuwaadhibu wachezaji hao hasa pale alipokuwa akikaripiwa na wachezaji mara baada ya kupuliza kipenga kuashiria ni makosa yametendeka.
Hadi kipindi cha kwanza kinaisha hakuna alieona lango la mwenzake. Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi huku Kusini Soccer ikionyesha Kandanda safi lakini walishindwa kutumia nafasi walizopata.
Refarii alivunja ukimwa Pale alipowatoa wachezaji wawili kwa kadi nyekundu kwa kosa la kupigana uwanjani na kufanya Timu zote kubaki pungufu ya Mchezaji mmoja kila upande.
Kwa upande wa Kariakoo Mchezaji Abdallah Jumanne na wa Kusini Soccer Mwalami Walishindwa kumaliza mchezo kwa uzembe huo wa kufanya fujo uwanjani.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.